MECHI ZA MWISHO ZA LIGI KUU ZENJ ZAPELEKEA KUBADILIKA KWA RATIBA ILI KUEPUSHA KUPANGA MATOKEO
Ligi kuu soka ya Zanzibar Kanda ya Unguja imebakisha
mizunguko miwili ili kumalizika lakini homa kali zaidi ni kila mmoja anataka
kujua ni timu gani ambazo zitafanikiwa kucheza 8 bora na timu zipi 6 ambazo
zitateremka daraja katika hatua ya awali.
Leo Kamati Tendaji ya ZFA Unguja imeamua kufanya mabadiliko madogo ya ratiba
baada ya kupokea agizo kutoka kwa uongozi wa uwanja wa Amaan sambamba na
kuepusha upangaji wa matokeo.
Mabadiliko ambayo yamefanywa yamepelekea siku ya Ijumaa ya
April 28, 2017 kuchezwa michezo mitatu ambapo KMKM watasukumana na Malindi saa
10:00 za jioni katika Uwanja wa Amaan ambapo muda huo huo katika Uwanja wa
Fuoni watacheza kati ya Kipanga dhidi ya KVZ , na mchezo wa Chuoni dhidi ya
Taifa ya Jang’ombe utapigwa saa 1:00 za usiku katika Uwanja wa Amaan.
Siku ya Jumamosi ya April 29, 2017 utapigwa mchezo mmoja
katika Uwanja wa Fuoni saa 10:00 za jioni kati ya Kijichi dhidi ya Polisi.
Mei 4, 2017 kutapigwa michezo miwili saa 10:00 za jioni
katika uwanja wa Fuoni Black Sailors dhidi ya Mundu, na saa 1:00 za usiku
katika Uwanja wa Amaan watasukumana kati ya Jang’ombe dhidi ya Mafunzo.
Timu 2 kati ya nne zilizojihakikishia kutinga hatua ya 8 bora
kutoka kanda ya Unguja ni kinara JKU yenye alama 69, Jang’ombe Boys alama 66
huku Taifa ya Jang’ombe iliyopo nafasi ya tatu na Zimamoto inayokamana nafasi
ya nne zote bado hazijajihakikishia kutinga hatua hiyo wakiwa na alama sawa 58
huku Polisi ambayo inakamata nafasi ya tano kwa alama 54 ikiwaombea dua Taifa
au Zimamoto kuharibu ili kupata wao nafasi hizo.
Timu 6 zilizokuwepo kwenye mstari mwekundu wa kushuka daraja
ni Malindi, Mundu, Kijichi, Miembeni, Chwaka na Kimbunga ambapo moja tu kati ya
hizo ikijikaza na kuomba wajuu wake waharibu inaweza ikanusurika ambayo ni
Malindi.
Kikosi cha Black Sailors |
Comments
Post a Comment