WACHEZAJI WA 5 WA ZANZIBAR HEROES WAMEITWA TIMU YA TAIFA YA TANZANIA TAIFA STARS KWAAJILI YA MICHEZO MIWILI YA KIMATAIFA YA KALENDA YA FIFA.
Kocha mkuu wa timu ya taifa ‘Taifa Stars’ Salum Mayanga ametangaza
kikosi cha wachezaji 23 ambao wataingia kambini kwa ajili ya
maandalizi ya michezo miwili ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya DR Congo na
Algeria.
Wachezaji wa tano wa Zanzibar ni mlinda mlango Abdulrahman
Mohamed wa JKU, pamoja na viungo Mudathir Yahaya wa Singida United, Feisal
Salum wa JKU, Abdulaziz Makame wa Taifa ya Jang’ombe na Mohamed Issa wa Mtibwa Sugar.
Kikosi kamili kilichotangazwa na Mayanga
kinajumuisha wachezaji wafuatao: Magolikipa ni Aishi Manula, Abdulrahman
Mohamed na Ramadhani Kabwili.
Walinzi: Shomari Kapombe, Hassan Kessy, Gadiel
Michael, Kelvin Yondani, Erasto Nyoni na Abdi Banda.
Viungo: Hamisi Abdallah, Mudathir Yahaya, Said
Ndemla, Feisal Salum, Abdulaziz Makame, Mohamed Issa, Thomas Ulimwengu, Farid
Mussa, Shiza Kichuya, Ibrahim Ajib.
Washambuliaji: Mbwana Samatta, John Bocco, Simon
Msuva na Yahaya Zayd.
Mara ya mwisho Mayanga alitaja kikosi cha Stars
Oktoba 24, 2017 kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Benin, wapo wachezaji
ambao wametemwa kwenye kikosi kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kushuka kwa
viwango vyao pamoja na majeraha lakini pia kuna wachezaji wapya walioitwa baada
ya kufanya vizuri siku za karibuni.
Wachezaji walioitwa kwenye kikosi cha Stars ambao
hawakuwepo kwenye kikosi kilichoitwa kwa ajili ya mchezo dhidi ya Benin.
Abdulrahman Mohamed, Shomari Kapombe, Hassan Kessy,
Faisal Salum, Abdulaziz Makame, Thomas Ulimwengu, John Bocco, Yahaya Zayd na
Said Ndemla.
Wachezaji waliokuwepo kwenye kikosi kilichocheza
dhidi ya Benin lakini wameachwa kwenye kikosi kilichotajwa leo kutokana na
sababu tofauti.
Peter Manyika, Boniphace Maganga, Nurdin Chona,
Dickson Daud, Himid Mao, Mzamiru Yassin, Raphael Daud, Abdul Mohamed, Mbaraka
Yusuph, Yohana Mkomola.
Comments
Post a Comment