KMKM KUANDAA MASHINDANO YA RIADHA
Kikosi maalum cha kuzuia magendo Zanzibar (KMKM)
kimeandaa mashindano ya mbio za kilomita 10 ambazo zinatarajiwa kufanyika
Jumapili ya Oktoba 29 mwaka huu zitakazoanza Makao Makuu ya KMKM Kibweni na
kumalizia katika Viwanja vya Maisara.
Akizungumzia lengo la Mashindano hayo CDR
Hussein Mohd Seif ambae ni mkuu wa Mafunzo na Michezo KMKM amesema kila mwaka
wanaandaa mashindano hayo kwaajili ya kujenga mahusiano ya karibu kati ya KMKM
na jamii.
Nae Mwenyekiti wa Chama cha Riadha Zanzibar
Abdulhakim Cosmas Chasama amewapongeza KMKM kwa kuendeleza Mashindano hayo kila
mwaka kwani yanaibua vipaji vingi katika mchezo huo.
Comments
Post a Comment