MLANDEGE HOI KWA AMAN FRESH, KESHO KWEREKWE CITY NA GULIONI

Mchezo wa kwanza hatua ya 4 bora ligi daraja la pili Wilaya ya Mjini kati ya Mlandege dhidi ya Aman Fresh wameshindwa kutambiana baada ya kutoka sare ya 1-1 mchezo uliopigwa saa 1 za usiku katika uwanja wa Amaan.
Aman Fresh ndio wa mwanzo kupata bao katika dakika ya 51 kupitia Rashid Suleiman Said.
Bao la Mlandege limefungwa kwa penalti na Saleh Salum "Neymar" dakika ya 86.
Lakini munamo dakika ya 63 Mohd Abdallah "Edi Mundo" wa Mlandege alikosa penalti.
Mchezo mwengine utapigwa kesho Mei Mosi kati ya Gulion na Kwerekwe City mchezo ambao utapigwa majira ya saa 1 za usiku katika uwanja wa Amaan.
Mchezo huo ni wa kulipana kisasi kwani msimu huu timu hizo zilikutana Jumapili ya Disemba 4, 2016 katika hatua ya Makundi ambapo Gulioni alipigwa mabao 5-0 dhidi ya City, sasa sijui kesho itakuaje Gulioni atalipa kisasi au City ataendeleza ubabe.
Bingwa na Makamo Bingwa katika ligi hiyo watawakilisha Wilaya ya Mjini kwenda kucheza na Wilaya nyengine sita zikiwemo Magharibi “A”, Magharibi “B”, Kaskazini “A”, Kaskazini “B”, Kati na Wilaya ya Kusini kwa kucheza ligi ya Mabingwa wa Wilaya ambayo itakuwa na timu 14 huku timu 4 zikitafutwa kupanda Daraja la Pili Taifa Msimu ujao.
Wachezaji wa Amaan Fresh

Comments

Popular posts from this blog

HUYU NDIYE MCHEZAJI MWENYE REKODI YA KUFUNGA MAGOLI MENGI KWENYE MECHI YA TAIFA DHIDI YA BOYS

WACHEZAJI WA 5 WA ZANZIBAR HEROES WAMEITWA TIMU YA TAIFA YA TANZANIA TAIFA STARS KWAAJILI YA MICHEZO MIWILI YA KIMATAIFA YA KALENDA YA FIFA.

KMKM KUANDAA MASHINDANO YA RIADHA