SINA TAARIFA ZOZOTE ZA KUFUNGIWA MAISHA NISIJIHUSISHE NA SOKA, KAMA WAMEFANYA HIVYO ZFA, HUO NI UHUNI-HUSSEIN
InakaribiaWiki moja sasa tangu kufungiwa kwa wajumbe wawili
wa ZFA Taifa kutoka Wilaya ya Mjini Hussein Ali Ahmada na Masoud Attai kutoka
Wilaya ya Kazkazini “A” ambao wote kwa pamoja wametimuliwa ndani ya Chama cha
Soka Visiwani Zanzibar “ZFA” na kusimamishwa maisha kutojihusisha na shughuli
za soka, leo yameibuka mapya kutoka kwa Hussein ambae amesema hana taarifa
rasmi za kufukuzwa kwake na yeye anajua bado ni Mjumbe wa ZFA Taifa kutoka ZFA
Wilaya ya Mjini.
Amesema amesikia kwenye vyombo vya habari tu kama amefungiwa lakini
hajapewa uthibitisho wowote na ZFA na kama wamefanya hivyo ZFA kitendo hicho ni
uhuni tu.
“Mimi nimesikia tu kwenu Waandishi, lakini sijapewa taarifa
rasmi mpaka leo, hivyo mimi taarifa hizo sijazielewa, kwasababu ukifungiwa
upewe barua maalum na ujuwe sababu gani zilizopelekea mimi kufungiwa, kama mimi
nimesimamishwa si tatizo lakini nipewee taarifa rasmi na wafate taratibu, mana
sielewi hata katiba gani ambayo wametumia kunisimamisha kama munavyosema,
lakini mimi niseme ZFA wanafanya maamuzi kipuuzi”. Alimalizia Hussein.
Jumamosi iliyopita ya April 22, 2017 Mkutano Mkuu wa dharura wa ZFA uliofanyika
Gombani Kisiwani Pemba uliwafukuza wajumbe wake wawili Hussen Ali Ahmada na
Massoud Attai na kuwafungia maisha kutojihusisha na Soka kutokana na sababu
tofauti moja wapo ikiileza kuwa viongozi hao walifanya vitendo vya ubadhirifu
wa mali wakati walipoongoza ZFA kwa muda baada ya chama hicho kupelekwa
Mahakamani.
Hussein Ali Ahmada |
Comments
Post a Comment