RAZA LEE AWAPA TAFU MABINGWA WATETEZI WA ROLLING STONE
Mwana michezo Mohd Ibrahim “Raza Lee” ambae ni mtoto wa
Mbunge wa Jimbo la Kiemba Samaki Ibrahim Raza asubuhi ya leo ameisaidia mipira
timu ya kombain ya Mjini Unguja ambao ni Mabingwa watetezi wa Mashindano ya Vijana ya Rolling
Stone, Mashindano ambayo yanatarajiwa kuanza rasmi June 29, 2017 na kumalizika
July 9, 2017 jijini Arusha.
Mipira hiyo Raza Lee ameikabidhi timu hiyo Dukani kwake ambalo
ni Duka la Vifaa vya Michezo ambapo Ali Othman “Kibichwa” Meneja wa Timu hiyo
pamoja na Mohammed Seif “King” kocha wa timu hiyo ndio waliyopokea Mipira hiyo.
Mohd Ibrahim "Raza Lee" akiwakabidhi Mipira Ali Othman "Kibichwa" Meneja na Mohammed Seif "King" Kocha |
Comments
Post a Comment