ALICHOKISEMA CAPTAIN SANGULA BAADA YA KUSAJILIWA NDANDA
Mlinzi wa kati Ibrahim Mohammed “Sangula” aliyekuwa anakipiga
katika klabu ya Jang’ombe Boys, amejiunga rasmi na klabu ya Ndanda FC kwa mkataba
wa miaka 2 ambapo kesho Jumanne Agost 1, 2017 akitarajiwa kuondoka Visiwani
Zanzibar kuelekea Mtwara ilipo klabu yake hiyo mpya.
Sangula ambae ndie Captain wa Jang’ombe boys amewashukuru
wadau wote wa soka Visiwani Zanzibar kwa ushirikiano wao huku akisisitiza
hawezi kumsahau kocha wake Issa Amasha na ataendelea kuipenda Boys licha ya
kuhama.
“Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kusajiliwa na Ndanda FC,
lakini nampongeza sana kocha wangu Amasha kwa kunilea vizuri kipindi chote
mpaka sasa nimesajiliwa kucheza ligi ya bara, naipenda sana Jang’ombe boys
lakini ndio maisha ya soka hutodumu timu moja naenda kutafuta maisha kwengine,
nawaomba waniombee dua ili mimi na Wazanzibar wengine tunacheza soka tufanikiwe
kutimiza ndoto zetu”. Alisema Sangula.
Sangula alionekana sana katika Mashindano ya Kombe la
Mapinduzi pamoja na Mashindano ya Sportpesa akiwa nahodha wa timu ya Jang’ombe
boys na vilabu vingi vilivutiwa na uchezaji wake jinsi anavyocheza.
Comments
Post a Comment