HAT TRICK 2 ZAPIGWA PEMBA LIGI KUU ZENJ, SASA HILIKA AFUNIKWA KWENYE UFUNGAJI BORA
Abdull Yussuf wa Mwenge |
Mshambuliaji wa timu ya Jamhuri Mwalimu Mohammed leo
amefanikiwa kufunga mabao 3 (Hat trick) katika mchezo wa ligi kuu soka ya
Zanzibar hatua ya 8 bora na timu yake Jamhuri iliposhinda mabao 5-3 dhidi ya
Mwenge kwenye mchezo uliopigwa jioni ya leo katika uwanja wa Gombani Pemba.
Mabao hayo amefunga katika dakika ya 11, 15, 27 ambapo katika
mchezo huo huo mshambuliaji wa timu ya Mwenge Abdull Yussuf nae amelipa hat
trick baada ya kufunga mabao yote 3 ya Mwenge katika mchezo huo waliopoteza
mabao ambayo alifunga dakika ya 33, 37 na 79.
Washambuliaji hao wote wawili kwasasa ndio vinara wa
kuzifumania nyavu katika ligi hiyo ambapo wote wakiwa na jumla ya mabao 7 kila
mmoja wakifuatiwa na Ibrahim Hamad Hilika wa Zimamoto mwenye mabao 6 baada ya
leo kufunga bao moja timu yake ilipotoka sare ya 1-1 dhidi ya JKU kwenye uwanja
wa Amaan.
Comments
Post a Comment