KOCHA MOROCCO AMUONGEZA EMANUEL MARTIN ZANZIBAR HEROES
Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Soka ya Zanzibar (Zanzibar Heroes),
Hemed Suleiman (Morocco) amemuongeza kwenye kikosi kiungo Mshambuliaji wa timu
ya Yanga Emanuel Martin ili kuzidi kuipa nguvu timu hiyo itakayokwenda Kenya
katika Mashindano ya CECAFA Chalenj CUP yanayotarajiwa kuanza Disemba 3-17,
2017.
Katika uteuzi wa awali Martin hakuitwa lakini kocha Morocco
amelazimika kumuongeza mshambuliaji huyo na atakuwa mchezaji wa 31 kwenye
kikosi cha Heroes kabla ya kubla ya kuchujwa na kubakia 24 ambao wanatarajia
kuondoka Zanzibar Jumatano ya Novemba 29.
Martin ambae ni mchezaji wa zamani wa JKU ya Zanzibar ataungana na
wenzake Ahmed Ali "Salula" (Taifa ya Jang'ombe), Nassor Mrisho
(Okapi), Mohammed Abdulrahman "Wawesha" (JKU), Abdallah Haji
"Ninja" (Yanga), Mohd Othman Mmanga (Polisi), Ibrahimm Mohammed
"Sangula" (Jang'ombe Boys), Adeyum Saleh "Machupa" (Kagera
Sugar), Haji Mwinyi Ngwali (Yanga), Abubakar Ame "Luiz" (Mlandege),
Issa Haidar "Mwalala" (JKU), Abdulla Kheir "Sebo" (Azam) na
Ibrahim Abdallah (Taifa ya Jang'ombe).
Wengine ni Abdul-swamad Kassim (Miembeni City), Abdul Aziz Makame
(Taifa ya Jang'ombe),Mudathir Yahya (Singida United), Omar Juma
"Zimbwe" (Chipukizi), Mohd Issa "Banka" (Mtibwa Sugar),
Amour Suleiman "Pwina" (JKU), Mbarouk Marshed (Super Falcon), Hamad
Mshamata (Chuoni), Suleiman Kassim "Seleembe" (Majimaji), Kassim
Suleiman (Prisons), Matteo Anton (Yanga), Ali Badru (Taifa ya Jang'ombe), Feisal
Salum (JKU), Salum Songoro (KVZ), Khamis Mussa "Rais" (Jang'ombe
boys), Mwalimu Mohd (Jamhuri), Seif Abdallah “Karihe” (Lipuli) na Ibrahim Hamad
Hilika (Zimamoto).
mbona jeba simuoni hapo kuongezwa au bado mbigili inamuhusu?
ReplyDelete