MZEE ZAM AULA CECAFA
Makamo
wa Rais wa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA Unguja) Mzee Zam Ali ameteuliwa kuwa
mjumbe katika kamati itakayosimamia Mashindano ya Chalenj CUP yaliyoandaliwa na
Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) Mashindano ambayo yanayotarajiwa
kuanza rasmi Disemba 3-17, 2017 nchini Kenya.
CECAFA
wamemteuwa Mzee Zam kwakuwa ni mzowefu katika Mashindano hayo ambapo ni
Mzanzibar pekee kwenye kamati hiyo.
Wengine
waliochaguliwa katika kamati hiyo ni Mutasim Gafar (Sudan), Abdigaan Arab Said
(Somalia), Jacob Odundo (Kenya), Ashinafi Ejigu (Ethiopia), Aimable Habimana
(Burundi), Rogers Byamukama (Uganda), Ajong Domasio Ajong (Sudan ya Kusini) na
Ahmed Mgoyi (Tanzania Bara).
Wengine
ni Sunday Kayuni (Tanzania Bara), Mossi Yussuf (Burundi), Celestine Ntangugira
(Rwanda), Yigzaw Ambaw (Ethiopia), Bernard Mfubusa (Burundi), Maxim Itur
(Kenya), Rogers Mulindwa (Uganda), Bonny Mugabe (Rwanda), Gishinga Njoroge (Kenya),
Amir Hassan (Somalia) na Nicholas Musonye (Kenya).
Comments
Post a Comment