WACHEZAJI 24 WA ZANZIBAR HEROES WATAKAOKWENDA KENYA KESHO CHALENJ CUP HAWA HAPA

Timu ya Taifa ya Soka ya Zanzibar (Zanzibar Heroes)  itaondoka nchini kesho Alhamis kuelekea Nairobi, Kenya kwa basi tayari kushiriki mashindano ya CECAFA Chalenj CUP yanayotarajiwa kuanza rasmi Disemba 3-17, 2017.

Jumla ya msafara wa watu 34 wakiwemo viongozi pamoja na wachezaji 24 wataondoka saa 6 za mchana kwa Boti kisha wakifika Dar es salam watapanda Basi kwenda mpaka Mkoani Tanga watalazimika kulala hapo, kisha asubuhi yake kuanza safari nyengine mpaka Mombasa na wakifika Mombasa watapanda Treni mpaka Nairobi.

Wachezaji 24 waliochaguliwa kuwakilisha kikosi hicho ni :-
WALINDA MLANGO
Ahmed Ali "Salula" (Taifa ya Jang'ombe), Nassor Mrisho (Okapi) na Mohammed Abdulrahman "Wawesha" (JKU).
WALINZI
Abdallah Haji "Ninja" (Yanga), Mohd Othman Mmanga (Polisi), Ibrahimm Mohammed "Sangula" (Jang'ombe Boys), Adeyum Saleh "Machupa" (Kagera Sugar), Haji Mwinyi Ngwali (Yanga), Issa Haidar "Mwalala" (JKU), Abdulla Kheir "Sebo" (Azam) na Ibrahim Abdallah (Taifa ya Jang'ombe).

VIUNGO
Abdul-swamad Kassim (Miembeni City), Abdul Aziz Makame (Taifa ya Jang'ombe),Mudathir Yahya (Singida United), Mohd Issa "Banka" (Mtibwa Sugar), Amour Suleiman "Pwina" (JKU) na Hamad Mshamata (Chuoni).
WASHAMBULIAJI
Suleiman Kassim "Seleembe" (Majimaji), Kassim Suleiman (Prisons),  Feisal Salum (JKU),  Khamis Mussa "Rais" (Jang'ombe boys), Mwalimu Mohd (Jamhuri), Seif Abdallah “Karihe” (Lipuli) na Ibrahim Hamad Hilika (Zimamoto).

Awali wachezaji hao walikuwa 30 na kulazimika kuachwa 6 ambao wengine waliachwa kwasababu ya majeruhi akiwemo Matteo Anton (Yanga), Ali Badru (Taifa ya Jang'ombe), Salum Songoro (KVZ) na Abubakar Ame "Luiz" (Mlandege) huku wengine walioachwa ni Mbarouk Marshed (Super Falcon) na Omar Juma "Zimbwe" (Chipukizi).

Comments

Popular posts from this blog

HUYU NDIYE MCHEZAJI MWENYE REKODI YA KUFUNGA MAGOLI MENGI KWENYE MECHI YA TAIFA DHIDI YA BOYS

WACHEZAJI WA 5 WA ZANZIBAR HEROES WAMEITWA TIMU YA TAIFA YA TANZANIA TAIFA STARS KWAAJILI YA MICHEZO MIWILI YA KIMATAIFA YA KALENDA YA FIFA.

KMKM KUANDAA MASHINDANO YA RIADHA