ZANZIBAR HEROES KUAGWA KESHO NA WAZIRI WA MICHEZO
Timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes), inatarajia kuagwa kesho kwa ajili ya safari yao ya kwenda
mjini Kenya, kwenye Mashindano ya CECAFA Chalenj CUP yanayotarajiwa kuanza
Disemba 3-17, 2017.
Heroes itaagwa saa
9:00 alaasiri na Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na michezo Rashid Ali Juma
katika ukumbi wa V.I.P Uwanja wa Amaan.
Katika Mashindano hayo Heroes imepangwa Kundi A
ambalo lina timu za Tanzania Bara, Libya, Rwanda na wenyeji Kenya.
Comments
Post a Comment