SIRI KUBWA KWETU KUFANYA VIZURI ZANZIBAR HEROES KWENYE CECAFA NI UMOJA :ABDUL AZIZ
Kiungo wa
Timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) Abdul aziz Makame (Abui) ameweka
hadharani siri kubwa iliyowapelekea kufanya vyema katika Mashindano ya
Cecafa Senior Challenge Cup
yanayoendelea nchini Kenya.
Makame amesema
umoja wao ndio silaha kubwa kwao mpaka wakafanikiwa kutinga fainali katika
Mashindano hayo.
“Sisi
tunapendana sana, yani tuna umoja wa hali ya juu sote wachezaji, viongozi mpaka
Mashabiki wetu, tunapokosea tunafahamishana kwa lengo la kutengeneza si kubomoa
ndio maana sasa tumefika fainali”. Alisema Makame.
Makame alichaguliwa
kuwa nyota wa mchezo (Men of the Match) katika mchezo wa nusu fainali ya pili
kati ya Zanzibar na Uganda ambapo Zanzibar ilishinda 2-1 na kesho Jumapili saa
9:00 Alaasiri Zanzibar itacheza fainali na wenyeji Kenya mchezo utakaopigwa
katika uwanja wa Kenyatta uliopo Machakos nchini Kenya.
Comments
Post a Comment