UCHAGUZI WA ZAHA UMEWIVA, FEBRUARY 18
Chama cha Mpira wa mikono Zanzibar (ZAHA)
kitafanya Uchaguzi wake ambao unatarajiwa kufanyika February 18, 2018.
Akizugumza na Mtandao huu Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi
Said Ali Mansabu amewataka wadau mbali mbali wa michezo kujitokeza kwa wingi
kuchukua fomu kugombea nafasi tofauti kwenye chama hicho.
Amesema baadhi ya wadau wanapenda kuwalaumu vingozi hivyo
hiyo ni fursa kwao kuja kugombea nafasi katika chama chama hicho.
“Mimi nawaomba wanamichezo wenzangu hasa wale wanoumwa na
Handa ball, wajitokeze kwa wingi kuchukua fomu katika chama hichi ili kupunguza
yale malalamiko ambayo watu wanasema viongozi wana matatizo wa chama hichi basi
hii ni fursa ya kupata viongozi wapya”. Alisema Mansabu.
Viongozi wapya watakaopatikana katika uchaguzi huo watakaa
madarakani kuanzia mwaka 2018 hadi 2022.
Comments
Post a Comment