MASHINDANO YA KIMATAIFA YA RESI ZA BASKELI KUFANYIKA KESHO ZANZIBAR
Wizara
ya Habari Utalii na Mambo ya Kale imeandaa Mashindano ya resi za Baskeli kwa
lengo la kuutanganza Utalii Visiwani Zanzibar.
Akizungumza
katika mkutano na waandishi wa habari ikuhusiana na matayarisho hayo katibu mtendaji wa Kamisheni ya Utalii
Dk Vuai Iddi amesema mashindano hayo yatajumuisha
waendesha baskeli vijana kutoka nchi mbali mbali za Afrika, hivyo amewata
wananchi kujitokeza kushangilia pamoja na kujionea uhondo wa mashindano hayo.
Amesea
mashindano hayo yatasaidia kuongeza idadi ya Watalii nchini na kuongeza pato la
taifa na wananchi mmoja mmoja pamoja na
ongeza la ajira kwa vijana.
Rais
wa vijana wa Afrika Mashariki Fest Peter
George Mzunda amesema lengo la mashindano hayo ni kutangaza utalii pamoja na
kuwapa fursa vijana kushiriki michezo ya baskeli na kuamsha hamasa kwa vijana
kupata ajira kupitia mchezo huo.
Katibu
mkuu wa Chama cha baskeli Zanzibar amesema kwa upande wa chama chao wameshukuru
kupata nafasi ya kushiriki mchezo huo huku akisema wao wameweza kufanya mchujo
na kuwapata wachezaji kumi kwa ajili ya mashindano hayo.
Akizungumza
kwa niaba ya mkuu wa Polisi wa Mkoa wa
Mjini Magharibi, Mkuu wa Trafiki wa
Wilaya ya Mjini msaidizi wa Polisi Moh’d
Talhata amesema kwa upande wa
Jeshi la Polisi limejipanga kiusalama ilikuhakikisha mashindano hayo
yanafanyika bila kuathiri shughuli za watu.
Mashindano
hayo ya Afrika Mashariki na kati kwa kilomita 60 yanatarajiwa kuanzia uwanja wa
Amani kupitia Mwera, Dunga, Jendele, Unguja Ukuu na kurejea kupitia barabara ya
Bungi, Fuoni, Mwanakwerekwe hadi uwanja
wa Amani huku Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Ayoub
Mohammed Mahamoud ambapo washiriki
watatokea Tanzania bara, Kenya, Uganda, Burundi na wenyeji Zanzibar huku
mataifa mengine yakialikwa katika Mashindano hayo wakiwemo Afrika ya Kusini, Zimbabwe,
Zambia na Swaziland.
Comments
Post a Comment