BINGWA WA LIGI KUU ZENJ HAJULIKANI ATAPEWA NINI, CENTRAL WILAYA YA MJINI WATATOA MILIONI 1 KWA BINGWA
Wajumbe wa Kamati ya Central W Mjini wakiwa pamoja na Mkanga (Aliyevaa Shati wa kati) |
Kamati ya central Wilaya ya Mjini imekabidhiwa
shilingi Milioni tatu kwaajili ya Zawadi kwa washindi 6 wa Mashindano yao ya
Ligi na ya Kombe la Mtoano yanayotarajiwa kumailizika Jumamosi ya Mei 12, 2018
asubuhi katika uwanja wa Amaan.
Akiwakabidhi fedha hizo Mkurugenzi wa Kampuni ya
Raskazone Trader Ali Khatib Mkanga amewaomba wadau wengine kujitokeza kusaidia
michezo hasa ngazi za chini kwani ndiko vipaji vinakotokea.
Mkanga pia amewapongeza viongozi hao wanaosimamia soka
la Vijana ndani ya Wilaya ya Mjini kwa mafanikio yao ya kusimamia vyema Soka
hilo la Vijana.
Nae katibu msaidizi wa Kamati ya Central Wilaya ya
Mjini Alawi Haidar Foum amempongeza Mkanga kwa kusaidia soka la Vijana huku
akiwataka watu wengine wasaidie Michezo hasa Vijana kwani ndio msingi imara wa
Maendeleo.
Kwa upande wake Makamo Mwenyekiti wa kamati hiyo Ali
Suleiman (Kisheta) amesema kamati yao imepanga kuanzisha Kombain kwa kila
daraja lao ili kuzidi kutoa ushindani kwa wachezaji kwani Wachezaji watajituma
zaidi kuhakikisha wanachaguliwa katika Kombain hizo.
Mashindano ya Central Ligi yatafungwa rasmi 12/05/2018
kwa kupigwa michezo mitatu katika Uwanja wa Amaan kwa kuchezwa fainali tatu za
kombe la Mtoano ambapo Daraja la Juvenile (U-14) watacheza kati ya Weles dhidi
ya Barcelona, daraja la Junior (U-17) watacheza kati ya New Afrika na Real Kids
huku kwa upande wa daraja la Central (U-21) watasukumana kati ya Mapembeani
dhidi ya King Boys.
Bingwa wa Mashindano hayo watazawadiwa fedha Taslim
Shilingi Milioni moja pamoja na zawadi nyengine ambapo mpaka sasa mabingwa kwa
upande wa ligi ni Sevilla (Juvenile), Barcelona (Junior) na Mapembeani
(Central) huku wakisubiriwa kwa hamu kubwa mabingwa wengine wa Kombe la Mtoano
Jumamosi.
Comments
Post a Comment