MKURUGENZI WA UFUNDI WA ZFA AOMBA KUJIUZULU HUKU KATIBU WA WIZARA YA MICHEZO AKITHIBITISHA ZFA WALIPOKEA BARUA KUTOKA CECAFA KWA LILE SWALA LA KARUME BOYS
Mkurugenzi wa Ufundi wa Chama cha Soka Visiwani
Zanzibar (ZFA) Abdulghan Msoma ameandika barua ya kujiuzulu nafasi yake baada
ya kukosa ushirikiano wa kutosha ndani ya chama hicho.
Msoma ameandika barua hiyo kwenda kwa Rais wa ZFA
ambapo amesema ZFA hakuna utendaji ndio mana kaamua kukaa pembeni huku akisema
wakati mwengine yanatoka maamuzi ambayo hayajajadiliwa katika vikao kwenye
chama hicho.
Nae katibu mkuu wa Wizara ya Vijana Sanaa Utamaduni na
Michezo Omar Hassan ‘King’ amesekiri kuwa ZFA wamethibitisha kupokea Barua
kutoka CECAFA kuhusu ufafanuzi wa umri wa Mashindano ya Vijana yaliyomalizika
hivi karibuni Burundi ambapo Zanzibar kupitia timu yao ya Karume Boys
iliondoshwa kutokana na kupeleka wachezaji waliozidi umri ambapo kwasasa mambo
yanaanza kufichukwa kwa kuwa kuna taarifa ya kuwa Makamo wa Rais ZFA Unguja
Mzee Zam Ali amesimamishwa kuhusu sakata hilo.
Zanzibar iliondolewa katika Mashindano hayo na
kupigwa faini kwa kosa la kuorodhesha wachezaji waliozaliwa kabla ya 01/01/2002
ambapo kanuni ya Mashindano hayo iliwataka wachezaji waliozaliwa kuanzia
01/01/2002 huku Zanzibar ikuwapeleka wachezaji 12 waliozaliwa 2001 jambo ambalo
ZFA wamesema hawana taarifa kama wachezaji walotakiwa waliozaliwa 2002 ambapo wao
walijuwa walokuwa na umri chini ya miaka 17 hivyo hata walozaliwa 2001 ikiwa
bado hawajafika miaka 17 walifikiri wanaruhusiwa ndio mana wakaenda nao ambapo
katibu Mkuu wa CECAFA Nicholaus Musonye alisema kuwa ZFA walitumiwa ufafanuzi
wa umri kwenye Barua Pepe labda hawazisomi tu.
Kutokana na makosa hayo Karume boys imepewa adahabu
tatu ikiwemo kuondolewa mashindanoni, inaambatana
na faini dola 15,000 (Sh 30 milioni) zinazotakiwa kulipwa na Chama cha Soka la
Zanzibar (ZFA), ambapo fedha hizo zitafidia gharama za tiketi, malazi na
chakula ya timu katika kipindi chote walichokaa Burundi huku adhabu ya tatu
ikiwa kufungiwa kutoshiriki mashindano yanayoendeshwa na CECAFA hadi hapo
watakapolipa faini hiyo ambayo inatakiwa kurudishwa FIFA.
Comments
Post a Comment