KAMATI TENDAJI YA ZFA YAVUNJWA, WENGINE WAPYA KUCHUKUA NAFASI
Mrajisi wa vyama vya michezo Zanzibar ameufungia uongozi wa kamati
tendaji ya ZFA ambao upo kwa mujibu katiba ya ZFA ya mwaka 2010 kwa kushindwa
kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa katiba yao.
Akizugumza na wandishi wa habari ukumbi wa uwanja wa Amani mjini Unguja
Sleman Pandu Kweleza amesema ofisi ya mrajisi wa vyama vya michezo Zanzibar
imefanya hivyo kwa mujibu wa sheria kwa kuwa ndio wanao simamia vyama vya
michezo vyote Zanzibar.
Akitoa sababu ya kufungia kamati hiyo mrajisi Pandu Kweleza amesema
baada ya kushindwa na kuupuza ombi la mrajisi la kutaka badhi ya vifungu vya
katiba yao ya ZFA kufanya marekebisho na kushindwa kufanya hivyo, aidha mrajisi
amefafanua alindakia barua kamati tendaji ya ZFA tarehe 20/3/2018 yenye kumbu
kumbu no BTMZ /MRJS/ VOLUME/10 ya kutaka kufanya marekibisho baadhi ya maeneo
ya katiba ya ZFA.
Aidha kwa upande mwengine mrajisi amesema kamati tendaji ya ZFA
imeshindwa kusimamia kanuni za michezo na kusababisha ligi kuu ya Zanzibar
kuonekana haina mvuto na kuzorota kwa mpira wa Zanzibar na kuupuza amri ya
mahakama kuu ya Zanzibar mwaka 2014 ya kutaka chama hicho kubadilisha katiba na
kuwa na Katiba inayoendana na CAF, ili kuondosha migogoro isiyo ya lazima.
“Niliwapa muda kufanya marekibisho toka tarehe 20 mwezi wa tatu hadi
tarehe 20/5 na kushindwa kufanya marekibisho lakini kamati hiyo ilipuuza ombi la
mrajisi ambaye ni msimamizi wa katiba za vyama vya michezo” Alisema Kweleza.
Hata hivyo mrajisi Kweleza ameteua kamati tendaji nyengine
itakayosimamia majukumu ya kamati tendaji ya ZFA kwa mujibu wa katiba ya ZFA
inayoundwa na wajumbe wafuatao :
Mwalim Ali Mwalim (Mwenyekiti).
Khamisi Abdalla Saidi ( Katibu).
Muhamed Hilali Muhamed (Katibu msaidizi).
Yussuf Muhamed Ali (Mjumbe).
Rajabu Juma Mtumweni (Mjumbe).
Mzee Ali Muhamedi (Mjumbe).
Abdulghani Abdalla Saidi (Mjumbe).
Kweleza amesema kamati hiyo mpya tendaji ya muda itatekeleza majukumu
yake kama yalivyoanishwa kwenye katiba ya ZFA aidha mrajisi amesema kamati hiyo
itatekeleza majukumu ya kusimamia upatikanaji wa Katiba mpya ya ZFA, kusimamia
mashindano yote zilizochini ya ZFA ikiwemo nane bora ya ligi kuu ya Zanzibar.
Aidha mrajisi amemalizia kwa kusema viongozi wa wilaya watendelea na
majukumu yao ya kawaida ila watakuwa chini ya kamati tendaji mpya.
YpranglobZria_zu-2001 Jan Roberts https://wakelet.com/wake/W5rN3fO1EvCtPhyKqwRLU
ReplyDeleteeninjsonle
0magreXrae-wo Tiffany Dickerson https://www.edukidsweb.com/profile/Dinosaurkingarcadegamebattlefreedownload-EXCLUSIVE/profile
ReplyDeletemocukedic
temppogimwo_Fayetteville Joe Dawson ScreenHunter Pro
ReplyDeleteWinRar
Avid Pro Tools
probosgigen
UrusconXid_hi Lisa Morgan Click here
ReplyDeletepremmulgmentwhee