KISANDU ATEULIWA KUWA MSEMAJI MPYA WA KAMATI TEULE YA ZFA
Na: Ibrahim Makame, Zanzibar.
Kamati teule
inayosimamia shughuli zote za Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) imepata msemaji wao
mpya ambae ni Abubakar Khatib Kisandu muandishi na mtangazaji wa michezo wa
Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC).
Akithibitisha
kuteuliwa kwake Kisandu amesema kweli amepokea barua kutoka kwa Katibu msaidizi
wa kamati hiyo Muhamed Hilali Tedy ya tarehe 7 mwezi Agost yenye namba
ZFA/KM/141/VOL/4 kutoka ofisi ya ZFA Taifa.
Aidha Kisandu
amekubali uteuzi huo na kuwaomba wadau wa michezo kumuunga mkono kwenye kipindi
chote cha miezi sita ya utumishi wake ndani ya kamati teule hiyo kwa kuwa wapo
kwenye kipindi cha kusimamia mpira wa Zanzibar.
Kwa Upande mwengine
kisandu amewataka wandishi wenziwe wa michezo kuumpa ushirikiano kwa kuwa yupo
katika majukumu mazito ya kitaifa ya kuusemea mpira wa Zanzibar ambao kimsingi
umekuwa na Changamoto nyingi sana.
“Nafurahi uteuzi
huu kwa kuwa ni mwanamichezo na muomba mungu anisaidie kwenye jukumu hili na
nawaomba sana wandishi wa michezo na wandishi wote waniunge mkono sisi ndio
wenye dhamana ya kufikisha mbali mpira wetu” Alisema Kisandu.
Abubakar Kisandu
amengia kwenye orodha hii ya wateule wajumbe na kubeba nafasi ya msemaji wa
kamati hiyo teule, kabla ya hapo ZFA ilikuwa na msemaji Ali Bakari Cheupe ambae
alikuwa anafanya kazi zote za Afisa Habari wa Chama hicho.
Comments
Post a Comment