Posts

Showing posts from September, 2018

MALINDI WAFANYA UCHAGUZI, MOHAMMED MASOUD NA MOHD ABDALLAH WAREJEA KAMA KAWAIDA

Timu ya Soka ya Malindi Sports Club imefanya uchaguzi wake mkuu na kuwapata viongozi wapya watakaoongoza timu hiyo kwa miaka minne ijayo. Katika Uchaguzi huo uliofanyika kwenye Ukumbi wa Empire Darajani Mjini Unguja, Mohd Abdallah Mohd amechaguliwa kuwa Mwenyekiti, Mohammed Masoud Rashid yeye ameshinda kuwa Katibu Mkuu ambapo Amir Saleh amechaguliwa kuwa Mhasibu huku Mshika Fedha Mkuu akichaguliwa kuwa Ali Majid na msaidizi Mshika Fedha ameshinda Rajab Said. Wengine walioshinda katika uchaguzi huo ni Jaffar Hussein Babu (Jeff) kuwa Makamo Mwenyekiti ambapo Naibu Katibu ameshinda Sefu Mussa wakati Abdallah Thabit (Dulla Sunday) kuwa Katibu Mwenezi ambapo waliochaguliwa kuwa Wajumbe wa kamati Tendaji ya timu hiyo ni Nassir Seif, Mustafa Ramadhan na Mahmoud Hamza. Akitangaza matokeo hayo msimamizi mkuu wa kamati ya Uchaguzi huo Omar Mohd Omar amesema Uchaguzi ulikuwa wa haki na huru ambapo wanachama wa timu hiyo walipata haki yao ya msingi kuchaguwa viongozi wao wapya watak...

ZFA YATOA KALENDA YA MWAKA

Image
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Kamati Teule ya Chama Cha Soka Visiwani Zanzibar (ZFA), imetoa kalenda ya msimu mpya wa mashindano na matukio mbali ya mchezo huo wa Soka kwa msimu wa mwaka 2018-2019. Kalenda inaonyesha kuanza na zoezi kwa vilabu kuwasilisha Majina ya wachezaji walioachwa  ambapo zoezi hilo tayari limeshaanza tangu Septemba 1 hadi 15 mwaka huu 2018. Kuanzia tarehe 16-27/09/2018 zoezi la uhamisho wa Wachezaji linaanza ambapo kuanzia tarehe 28/09/2018-05/10/2018 zoezi la usajili kwa Wachezaji litachukua nafasi wakati kuanzia tarehe 01-05/10/2018 itakuwa kipindi cha Refresh Course. Kwa mujibu wa Kalenda hiyo, kuanzia tarehe 06-10/10/2018 itakuwa ni siku za Pingamizi ya Usajili ambapo tarehe 10-15/10/2018 kutakuwa na zoezi la Copa Test kwa Waamuzi na Mafunzo ya Leseni kwa Vilabu. Tarehe 11-17/10/2018 ni siku za kupitia fomu na kutoa block Registration. Mchezo wa Ngao ya Jamii utachezwa tarehe 18/10/2018 ambapo ligi za madara yote yataanza kuanzia ta...