ZFA YATOA KALENDA YA MWAKA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kamati Teule ya
Chama Cha Soka Visiwani Zanzibar (ZFA), imetoa kalenda ya msimu mpya wa
mashindano na matukio mbali ya mchezo huo wa Soka kwa msimu wa mwaka 2018-2019.
Kalenda inaonyesha
kuanza na zoezi kwa vilabu kuwasilisha Majina ya wachezaji walioachwa ambapo zoezi hilo tayari limeshaanza tangu
Septemba 1 hadi 15 mwaka huu 2018.
Kuanzia tarehe
16-27/09/2018 zoezi la uhamisho wa Wachezaji linaanza ambapo kuanzia tarehe
28/09/2018-05/10/2018 zoezi la usajili kwa Wachezaji litachukua nafasi wakati
kuanzia tarehe 01-05/10/2018 itakuwa kipindi cha Refresh Course.
Kwa mujibu wa
Kalenda hiyo, kuanzia tarehe 06-10/10/2018 itakuwa ni siku za Pingamizi ya
Usajili ambapo tarehe 10-15/10/2018 kutakuwa na zoezi la Copa Test kwa Waamuzi
na Mafunzo ya Leseni kwa Vilabu.
Tarehe
11-17/10/2018 ni siku za kupitia fomu na kutoa block Registration.
Mchezo wa Ngao ya
Jamii utachezwa tarehe 18/10/2018 ambapo ligi za madara yote yataanza kuanzia
tarehe 20/10/2018.
Tarehe 01/11/2018
Maandalizi ya timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) kwaajili ya
Mashindano ya Cecafa Senior Challenge Cup.
Tarehe
01-18/12/2018 Michuano ya Cecafa Senior Challenge Cup.
Tarehe 10/12/2018
Maandalizi ya Kombe la Mapinduzi.
Tarehe 25/12/2018
Mzunguko wa kwanza wa Ligi kuu kumalizika.
Tarehe
28/12/2018-13/01/2019 Michuano ya Kombe la Mapinduzi.
Tarehe
01-20/01/2019 Mapumziko ya Dirisha Dogo na Uhamisho.
Tarehe
21-25/01/2019 Usajili wa Dirisha Dogo.
Tarehe
26/01/2019-05/02/2019 Kupitia Fomu za Usajili na Kutoa Block Registration .
Tarehe 06/02/2019-29/05/2019
Kuendelea ligi mzunguko wa Pili.
Tarehe
01/03/2019-30/05/2019 FA Cup na Ligi za Mabingwa wa Wilaya Daraja la Pili.
Comments
Post a Comment