MALINDI WAFANYA UCHAGUZI, MOHAMMED MASOUD NA MOHD ABDALLAH WAREJEA KAMA KAWAIDA
Timu ya Soka ya Malindi Sports Club imefanya
uchaguzi wake mkuu na kuwapata viongozi wapya watakaoongoza timu hiyo kwa miaka
minne ijayo.
Katika Uchaguzi huo uliofanyika kwenye Ukumbi
wa Empire Darajani Mjini Unguja, Mohd Abdallah Mohd amechaguliwa kuwa
Mwenyekiti, Mohammed Masoud Rashid yeye ameshinda kuwa Katibu Mkuu ambapo Amir
Saleh amechaguliwa kuwa Mhasibu huku Mshika Fedha Mkuu akichaguliwa kuwa Ali
Majid na msaidizi Mshika Fedha ameshinda Rajab Said.
Wengine walioshinda katika uchaguzi huo ni Jaffar
Hussein Babu (Jeff) kuwa Makamo Mwenyekiti ambapo Naibu Katibu ameshinda Sefu
Mussa wakati Abdallah Thabit (Dulla Sunday) kuwa Katibu Mwenezi ambapo
waliochaguliwa kuwa Wajumbe wa kamati Tendaji ya timu hiyo ni Nassir Seif,
Mustafa Ramadhan na Mahmoud Hamza.
Akitangaza matokeo hayo msimamizi mkuu wa
kamati ya Uchaguzi huo Omar Mohd Omar amesema Uchaguzi ulikuwa wa haki na huru
ambapo wanachama wa timu hiyo walipata haki yao ya msingi kuchaguwa viongozi
wao wapya watakayoingoza timu hiyo ambayo itashiriki ligi kuu Soka ya Zanzibar
kwa msimu mpya wa mwaka 2018-2019.
Akizungumza mara baada ya kumalizika uchaguzi
huo Mwenyekiti mpya wa timu hiyo Mohd Abdallah Mohd amewataka Wanachama na
Mashabiki wote wa Malindi kuwa kitu kimoja ili timu yao kufanya vyema kwenye
ligi kuu soka ya Zanzibar na kupata nafasi ya kuiwakilisha Zanzibar katika
Mashindano ya Kimataifa.
Comments
Post a Comment