JABIR AENGULIWA, HUSSEIN AHMADA AKUBALI YAISHE UCHAGUZI WA ZFF
Mkurugenzi wa
Ufundi wa Kamati ya Olympik Tanzania (TOS), Suleiman Mahmoud Jabir, ambae
alikuwa anagombea nafasi ya urais kwenye Uchaguzi wa Shirikisho la Soka
Zanzibar (ZFF) ameondoshwa katika kinyang'anyiro hicho kwa kile kilichoelezwa kukiuka
taratibu za uchaguzi kwa kufanya kampeni kabla ya muda.
Akizungumza na
Kisanduzenj Makamo mwenyekiti wa kamati ya Uchaguzi Juma Msafiri Karibona amesema
Jabir wamemuondosha kwenye orodha ya wagombea nafasi ya Urais kutokana na
kwenda kinyume na masharti yaliyowekwa na kamati inayosimamia uchaguzi huo huku
Hussein Ahmad Vuai ambae alikuwa anagombea nafasi ya Makamo wa Urais amejitowa
mwenyewe kwenye kinyang'anyiro hicho.
‘’Mgombea
Suleiman Mahmoud tumemuondowa kwasababu kakosa sifa kwa vile tumejiridhisha
kaanza kufanya kampeni za kimakundi kabla ya muda wa kampeni, na hoja ya pili
tumegunduwa hana maadili mazuri, kwaiyo barua yake tayari
tumeshampa na tumemtoa rasmi’’.
Tulimtafuta
Suleiman Mahmoud baada ya kuondolewa kwenye mchakato huo amesema amesikitishwa
na kamati hiyo kumuundoa kwenye uchaguzi huo.
‘’ Kwa kweli
nasikitika kuona nchi yangu imenisomesha kwa mapenzi na mimi juhudi zangu za
kuendeleza masuala haya ya michezo hasa ngazi ya uongozi, ati sina sifa wakati
nimekuwa najulikana hapa Afrika na nje ya Afrika kwenye masuala haya ya uongozi
wa michezo, nimepokea barua ati inasema nimeaanza kampeni! Barua hiyo haina
ushahidi wowote ati nimeanza kampeni, barua haina ushahidi ya kusema kuna kikao
kilifanywa au tarehe Fulani, muda Fulani na watu Fulani nimepiga kampeni,
hahahhaha yani inachekesha sana’’. Alisema Suleiman.
Wagombea
waliopitishwa kwenye kinyang'anyiro hicho kwa ngazi Rais ni Khamis Abdallah
Said, Ame Abdallah Dunia na Seif Kombo Pandu wakati wanaowania nafasi ya Makamo
ni Khamis Shaali Chum na Salum Ubwa Nassor ambapo Uchaguzi huo unatarajiwa
kufanyika June 2, 2019 Kisiwani Unguja na sasa rasmi kampeni zimefunguliwa.
WbracerQde_gi1988 Cesar Padilla https://wakelet.com/wake/_0MJY5SdDNjSyvqEhuX2n
ReplyDeletelimpgensoundking