NINJA WA YANGA ASAINI TIMU ULAYA, APELEKWA KWA MKOPO LA GALAXY A KUCHEZA PAMOJA NA IBRAHIMOVIC
Mlinzi wa kati wa timu ya Yanga
Abdallah Haji Shaibu (Ninja) amejiunga na timu ya MFK Vyskov ya Jamhuri ya
Czech barani Ulaya kwa mkataba wa miaka 4.
Timu hiyo ambayo inashiriki ligi
Daraja la Tatu nchini humo imepanga kumtoa kwa mkopo kwenda kucheza kwenye
klabu ya LA Galaxy ambayo inashiriki ligi kuu Soka ya Marekani (MSL) ikiwa na
nyota kadhaa waliyowika Duniani akiwemo mchezaji wa zamani wa Barcelona, Inter
Milan na Manchester United Zlatan Ibrahimovic.
Meneja wa Mchezaji huyo Abubakar
Khatib Kisandu amesema tayari wameshamalizana na MFK Vyskov ambayo inashiriki
ligi Daraja la Tatu Jamhuri ya Czech ambapo atakwenda kwa mkopo Marekani
kucheza LA Galaxy.
Alipoulizwa kuhusu dili hilo
limekujaje Meneja Kisandu amesema kuna Kampuni ya Mawakala wa Wachezaji DreamWorld
Sports and Entertainment LLC Player ndio iliyomuona Mlinzi huyo kwenye Michezo
ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika msimu wa mwaka 2017-2018 akiitumikia Yanga
kwa mara ya kwanza na kufunga nao Mkataba ndipo ilipoamua kumpeleka Barani
Ulaya.
Ninja alijiunga na Yanga June 14,
2017 kwa mkataba wa miaka 2 ambapo baada ya kumalizika mkataba wake mwaka huu
ndipo alipoamua kwenda kucheza Soka Barani Ulaya.
Nice sana hii. kapige kazi mwanangu
ReplyDeleteBlessing ninja
ReplyDelete