UFAFANUZI JUU YA MCHEZAJI SHAIBU NINJA KUSAJILIWA MAREKANI LA GALAXY
Wadau wengi wa Soka hapa Zanzibar na Tanzania
Bara wanahamu sana kujua juu ya hatma ya Beki wa zamani wa Yanga Abdalla Haji
Shaibu (Ninja) kuhusu kwenda kucheza Soka nchini Marekani.
Ni kweli Ninja sasa yupo Marekani kwenye timu
ya La Galaxy ambapo amekwenda kwa mkopo, na baada ya kufanyiwa vipimo vya afya
na mambo mengine La Galaxy wamelazimika kumuweka timu ya La Galaxy II (Timu B)
na baada ya kuonekana anahitaji kuzowea mazingira na kupata uzoefu kidogo
kwenye timu hiyo B kisha watampandisha kucheza timu kubwa ambayo inashiriki
ligi kuu Soka Marekani, timu ambayo anacheza Zlatan Ibramovic.
Ninja tayari ameshaanza mazoezi kwenye timu
hiyo B na uzuri kwamba timu hiyo B wakati mwengine wanachanganyika kufanya
mazoezi na timu kubwa kwasababu muda wowote mchezaji wa timu B akionyesha
kiwango hupandishwa timu kubwa.
Ninja amepewa jezi no 51, hivyo naomba
Watanzania wafahamu kuwa kijana wao alikusudiwa kwenda kwa mkopo kwenye timu
kubwa lakini kutokana na kutofanya mazoezi kipindi kirefu tangu kumaliza ligi
kuu soka Tanzania bara msimu uliopita Mei 28, 2019 mpaka juzi anafika Marekani
hakuwa fit kucheza timu ya Primier kwani kwani zaidi ya miezi mitatu hakufanya
mazoezi imara ya pamoja na ukiangalia ligi ya Marekani inaendelea.
Naomba tena Watanzania wafahamu Ninja amesajiliwa Timu a MFK Vyskov ya Jamhuri ya Czech barani Ulaya kwa
mkataba wa miaka 4 lakini timu yake hiyo ambayo inashiriki ligi Daraja la Tatu
nchini humo ndiyo imemtoa kwa mkopo wa mwaka mmoja kwenda kucheza kwenye klabu
ya LA Galaxy Marekani lakini sivyo tulivyotegemea acheze LA Galaxy ambayo
inashiriki ligi kuu Soka ya Marekani (MSL) ikiwa na nyota kadhaa waliyowika
Duniani akiwemo mchezaji wa zamani wa Barcelona, Inter Milan na Manchester
United Zlatan Ibrahimovic, ila mambo yamekwenda vyengine kidogo kwa kuekwa timu
B.
Naomba niwafahamishe tena Watanzania timu B si timu
ndogo, timu B ina thamani kubwa sana kwani wakati wowote kukilazimika kuongezwa
mchezaji anapandishwa na wakati mwengine wanafanya mazoezi na timu kubwa hivyo
si hatua ndogo Ninja kutoka Yanga mpaka kucheza La Galaxy II nchini Marekani na
kubwa ni kumuombea dua afanikiwe kwani akifanikiwa yeye ndio kutufungulia njia
Watanzania wengine kupata nafasi.
Kwa wale ambao wanasema Ninja hajaenda La Galaxy ya
Marekani wafunguwe link hiyo wataona La Galaxy wenyewe walivyomuweka
Comments
Post a Comment