4 BORA DARAJA LA PILI WILAYA YA MJINI KUANZA APRIL 30, MLANDEGE, KWEREKWE CITY, GULIONI NA AMAN FRESH KUPIGANA
Hatua ya nne bora ligi Daraja la Pili Wilaya ya Mjini ambapo
wanatafutwa Bingwa na Makamo Bingwa wa Wilaya hiyo watakaowakilisha katika
Mabingwa wa Wilaya kupigania nafasi za kupanda daraja la 2 Taifa kwa msimu
ujao, ligi hiyo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi lake April 30, 2017 kati ya timu
ya Mlandege dhidi ya Amani Fresh mchezo ambao utapigwa saa 1 ya usiku.
Mchezo mwengine utapigwa Mei Mosi kati ya Gulion na Kwerekwe
City mchezo ambao utapigwa majira ya saa 1 za usiku katika uwanja wa Amaan.
Akizungumza na Mtandao huu Katibu wa ZFA Wilaya ya Mjini
Yahya Juma Ali amesema ligi yao itakuwa na ushindani mkubwa kwani timu zote 4
zilizofanikiwa ni ngumu.
“Hii 4 bora ya mwaka huu si mchezo kwa vile timu zote
zinaushindani wa hali ya juu”. Alisema Yahya.
Bingwa na Makamo Bingwa katika ligi hiyo watawakilisha Wilaya
ya Mjini kwenda kucheza na Wilaya nyengine sita zikiwemo Magharibi “A”,
Magharibi “B”, Kaskazini “A”, Kaskazini “B”, Kati na Wilaya ya Kusini kwa
kucheza ligi ya Mabingwa wa Wilaya ambayo itakuwa na timu 14 huku timu 4
zikitafutwa kupanda Daraja la Pili Taifa Msimu ujao.
Kikosi cha Kwerekwe City |
Kikosi cha Gulioni |
Comments
Post a Comment