BAO PEKEE LA RAIS WA BOYS LASAHAULISHA BENDERA YA MASHABIKI WA TAIFA AMAN

Baada ya jana timu ya Taifa ya Jang'ombe kufungwa bao 1-0 na Jang'ombe Boys kwenye mchezo wa ligi kuu soka ya Zanzibar uliopigwa Amaan,  baadhi ya Mashabiki wa timu hiyo wasahau bendera yao kiwanjani hapo.

Bao la dakika ya 86 lililofungwa na Khamis Mussa (Rais) ndilo lililopeleka kilio kwa Taifa na ndilo lililosababisha Bendera hiyo kusahauliwa. 

Wachezaji wa JKU ambao hufanya mazoezi katika uwanja wa Aman asubuhi ya leo wameishuhudia bendera hiyo iliyosahauliwa na mashabiki hao katika uwanja huo.

"Ni kweli tumeiona Bendera ya Mashabiki wa Taifa asubuhi ya leo iliyosahauliwa jana usiku".Kilieleza chanzo.

Taifa ya Jang'ombe na Jang'ombe boys ni mahasimu sana,  jambo ambalo linapelekea kwa timu itakayofungwa baadhi ya mashabiki wao kushindwa hata kula na kufanya mambo mengine.

Comments

Popular posts from this blog

HUYU NDIYE MCHEZAJI MWENYE REKODI YA KUFUNGA MAGOLI MENGI KWENYE MECHI YA TAIFA DHIDI YA BOYS

WACHEZAJI WA 5 WA ZANZIBAR HEROES WAMEITWA TIMU YA TAIFA YA TANZANIA TAIFA STARS KWAAJILI YA MICHEZO MIWILI YA KIMATAIFA YA KALENDA YA FIFA.

KMKM KUANDAA MASHINDANO YA RIADHA