DK SHEIN AHIMIZA WAZANZIBAR KUWA NA UZALENDO KWA KUIPENDA ZANZIBAR HEROES, HATA WAKIPENDA KINA ARSENAL LAKINI UZALENDO MUHIMU
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali
Mohamed Shein amewataka Wanaanchi wa Jimbo la Uzini kuwa na uzalendo wa kupenda
chao na kukithamini kwani mtu chake ambapo amewasisitiza kuipenda timu ya Taifa
ya Soka ya Zanzibar “Zanzibar Heroes”.
Dkt. Shein ameyasema hayo asubuhi ya leo huko Dunga Wilaya ya
Kati kwenye Ukumbi wa Walimu alipokuwa akiwakabidhi Vifaa vya Michezo timu 46
za soka za Jimbo la Uzini ambao wamepewa vifaa hivyo na Muwakilishi wao Mh Mohd
Raza.
Amesema katika uzalendo lazima uanze kukipenda chako huku
akiwanasihi Vijana hao kuipenda timu ya Taifa ya Zanzibar “Zanzibar Heroes”.
“Katika Uzalendo mtu hukipenda chake kwanza, hebu ipendeni
kwanza Zanzibar Heroes timu yenu ya Taifa ya Zanzibar, ipendeni Timu ya Jamhuri
ya Muungano Tanzania “Taifa Stars”, muzipende timu zenu huo ndio uzalendo”.
Alisema Dkt Shein.
Hata hivyo Dkt Shein amesisitiza kuwa hajamzuia mtu kupenda
klabu za Ulaya lakini mtu asipende sana cha nje akakisahau za kwao.
“Hazuiliwi mtu kupenda timu ya nje ya nchi yetu, anaependa Manchester
United, Arsenal, Chelsea, Liverpool sawa
tu, najuwa wapo hao! pendeni vile vile lakini musipende mwisho mkajisahau
mkaziponda timu zenu, pendeni zote hizo Barcelona, Real Madrid zote zipendeni
lakini bado muwe wazalendo wa timu zenu, zetu ndio bora, mukipenda vya nje sana
mutavisahau vyenu”. Alisisitiza Dkt Shein.
Zanzibar Heroes |
Rais wa Zanzibar Dkt Shein akiwakabidhi vifaa timu za Jimbo la Uzini |
Comments
Post a Comment