HOMA INAZIDI KUWA KALI LIGI KUU ZENJ YAKARIBIA KUMALIZIKA KUTAFUTA TIMU 8 BORA NA 12 ZAKUSHUKA DARAJA
Mzunguko wa 33 wa ligi kuu soka ya Zanzibar kanda ya Unguja
unatarajiwa kuanza rasmi kesho Ijumaa kwa kupigwa mchezo mmoja katika Uwanja wa
Amaan.
Ratiba ya mzunguko wa 33 ligi kuu ya soka Zanzibar kanda ya
Unguja hiyo.
Ijumaa 28/4 Taifa vs Chuoni saa 10:00 Amaan.
J/mosi 29/4 Polisi vs Kijichi saa 10:00 Fuoni
J/pili 30/4 Mafunzo vs Miembeni saa 8:00 Amaan
J/pili 30/4 JKU vs Mundu saa 10:00 Amaan
J/nne 02/5 Chwaka vs Zimamoto saa 8:00 Amaan
J/nne 02/5 B/Sailors vs Kimbunga saa 10:00 Amaan
J/nne 02/5 Kilimani C vs J/Boys saa 1:00 usiku.
Jumatano 3/5 KMKM vs Malindi saa 8:00 Amaan.
Jumatano 3/5 Kipanga vs KVZ saa 10:00 Amaan.
Timu 2 kati ya nne zilizojihakikishia kutinga hatua ya 8 bora
kutoka kanda ya Unguja ni kinara JKU yenye alama 69, Jang’ombe Boys alama 66
huku Taifa ya Jang’ombe iliyopo nafasi ya tatu na Zimamoto inayokamana nafasi
ya nne zote bado hazijajihakikishia kutinga hatua hiyo wakiwa na alama sawa 58
huku Polisi ambayo inakamata nafasi ya tano kwa alama 54 ikiwaombea dua Taifa
au Zimamoto kuharibu ili kupata wao nafasi hizo, lakini Taifa na Zimamoto wakishinda
mchezo mmoja tu kati ya hiyo miwili iliyobakia wanajihakikishia kutinga 8 bora
na Polisi hatoweza kuwafikia hata ashinde michezo yote yake miwili.
Kwa upande wa kanda ya Pemba timu 4 tayari zishajulikanwa
zilizotinga 8 bora ambazo ni Jamhuri, Mwenge, Kizimbani na Okapi zote kutoka Mkoa
wa Kaskazini Pemba.
Lakini homa nyengine kali ni upande wa kushuka daraja kanda
ya Unguja timu 5 kati ya 6 tayari zimeshajulikanwa za kushuka daraja katika
hatua ya awali huku moto mkali upo kwa Malindi ambae nae yupo katika mstari
mwekundu akimuombea mabaya Kipanga ambapo Kipanga mpaka sasa ameondoka kwenye
mstari huo mwekundu akishika nafasi ya 12 kwa alama 41 huku Malindi ambae yupo
kwenye mstari mwekundu nafasi ya 13 ana alama 39 na wote wakiwa wamebakiwa
michezo miwili mkononi.
Kikosi cha KVZ |
Kikosi cha Kipanga |
Comments
Post a Comment