IKRAM OMAR MJUMBE MPYA ZFA KWA MARA YA KWANZA KUINGIA KATIKA MKUTANO MKUU

Ikram Omar Mjumbe mpya wa ZFA Taifa kutoka Wilaya ya Kati

Mjumbe mpya wa ZFA Taifa kutoka Wilaya ya Kati Ikram Omar ambae pia ni Mtangazaji wa Michezo kupitia kipindi cha Coco Sports ya Coconut FM leo kwa mara ya kwanza ametinga katika Mkutano Mkuu wa ZFA uliofanyika Gombani Kisiwani Pemba.

Hivi karibuni Ikram amefanikiwa kushinda katika Uchaguzi mdogo wa ZFA Wilaya ya Kati kwa nafasi ya Mjumbe kwenda Taifa baada ya kumuangusha mpinzani wake Salum Hassan.

Kwasasa ndani ya ZFA kuna Waandishi wa Habari wawili akiwemo Ikram na Ali Bakar “Cheupe” ambae ni Afisa Habari wa chama hicho.

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

HUYU NDIYE MCHEZAJI MWENYE REKODI YA KUFUNGA MAGOLI MENGI KWENYE MECHI YA TAIFA DHIDI YA BOYS

WACHEZAJI WA 5 WA ZANZIBAR HEROES WAMEITWA TIMU YA TAIFA YA TANZANIA TAIFA STARS KWAAJILI YA MICHEZO MIWILI YA KIMATAIFA YA KALENDA YA FIFA.

KMKM KUANDAA MASHINDANO YA RIADHA