KAMATI YA KATIBA YA ZFA YAWATOWA HOFU WAZANZIBAR KUHUSU KATIBA WATAKAYOIREKEBISHA KUENDANA NA MATAKWA YA CAF
Kamati iliyoundwa kwa ajili ya kuifanyia marekebisho katiba
ZFA ili kuendana na matakwa ya Shirikisho la Soka Barani Afrika “CAF” inatarajia
kuiwasilisha rasimu ya awali ya katiba kwa takribani wiki mbili kwa Chama cha
Soka Zanzibar “ZFA”.
Akizungumza na kisanduzenj.blogspot.com katibu wa kamati hiyo
Saleh Ali Said ambae pia ni Mwanasheria wa ZFA amesema wameanza kazi za kuandaa
katiba hiyo ambapo jana Jumamosi wameanza kazi ya awali na zoezi hilo litachukua
muda mfupi tu kukamilika.
“Tushaanza kazi hiyo mana tumekutana wajumbe na zoezi hili si
kubwa sana, tutachukua wiki moja na nusu au mbili tu kukamilisha rasimu ya
awali ya katiba kisha tutaiwasilisha kwa ZFA, Wazanzibar wasiwe na hofu katiba
hiyo itakuwa inaendana na matakwa ya Shirikisho la Soka Afrika pamoja na kwa
maslahi ya Mazingira ya Visiwa vya Zanzibar”. Alisema Saleh.
Awali Kamati hiyo ilihitaji fedha kwaajili ya bajeti yao ili
kufanikisha zoezi hilo ambapo ilihitaji jumla ni shs Milioni thalasini na tisa
, laki nane na hamsini elfu (39,850,000/=) lakini zoezi hilo likashindwa
kufanyika kutokana na ZFA kushindwa kuwapatia fedha hizo ambapo kwasasa wameweka
uzalendo mbele na kukubali kufanya kazi hiyo bila ya fedha hizo baada ya ZFA
kupatiwa uanachama wa kudumu wa CAF sasa zoezi hilo litakuwa rahisi mno kuliko
awali kwani katiba inayotakiwa iendane na matakwa ya CAF.
Viongozi sita (6) waliochaguliwa kwenye kamati hiyo ni Afan
Othman Juma (Mwenyekiti), Saleh Ali Said (Katibu), Othman Ali Hamad (Msaidizi
Katibu), pia yumo Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Zanzibar ya soka la Wanawake
(Zanzibar Queens) Nassra Juma na wengine ni Eliud Peter Mvella na Ame
Abdallah Dunia.
Saleh Ali Said Mwanasheria wa ZFA |
Comments
Post a Comment