AFRICAN MAGIC YAWATESA KVZ, KOMBE LA MUUNGANO
Kikosi cha African Magic |
Mashindano ya Kombe la Muungano 2017 kwa mpira wa Kikapu
(Basketball) yameendelea tena saa 2 asubuhi
ya leo Jumatatu katika Uwanja wa Gmkhana ambapo timu ya African Magic ya
Wanawake ikafanikiwa kuwafunga Maafande wa KVZ kwa vikapu 72-31.
Mchezo mwengine umepigwa majira ya saa 4 za asubuhi katika
Uwanja huo ambapo walicheza Wanaume timu ya Stone Town dhidi ya Nyuki ambapo
Wana Jeshi wa Nyuki wakafanikiwa kushinda kwa vikapu 79-59.
Mechi nyengine za leo zote ni kwa upande wa Wanaume ambapo
mchezo unaoendelea sasaivi saa 6 za mchana ni kati ya Polisi dhidi ya JKT, na
saa 8 za mchana watakipiga timu ya Mbuyuni dhidi ya Tanado, saa 10 za jioni
African Magic dhidi ya Stone Town.
Kombe hilo litaendelea tena kesho Jumanne ya April 24, kwa
kupigwa mchezo mmoja tu saa 2 za asubuhi kwa Wanaume wa Tonado kutokea Tanzania
bara dhidi ya Chake ya Pemba ambapo watasukumana katika Uwanja wa Gmkhana.
Comments
Post a Comment