LIGI KUU ZENJ BADO INAWAKA MOTO MKALI, KMKM HOI KWA MAOSTADHI WA CHUONI
Wachezaji wa KMKM |
Ligi kuu soka ya Zanzibar kanda ya Unguja imeendelea tena leo kwa kupigwa michezo miwili tofauti ambapo saa 8:00 za mchana katika Uwanja wa Amaan mabaharia wa KMKM wakakubali kuchapwa bao 1-0 dhidi ya Maostadhi wa Chuoni.
Mchezo mwengine umepigwa saa 10 za jioni kiwanjani hapo baada
ya Mafunzo kuichapa Kijichi 2-0.
Lakini kwa upande wa kanda ya Pemba leo Chipukizi ilitoka na
ushindi mabao 5-1 dhidi ya Aljazeera huku Shaba wakiichapa New Star bao 1-0.
Ligi kuu soka ya Zanzibar kanda ya Unguja itaendelea tena
kesho kwa kupigwa michezo miwili katika Uwanja wa Amaan.
Saa 10:00 za jioni Mundu FC v/s Chwaka Stars, na saa 1:00
usiku ni zamu ya Polisi v/s Zimamoto.
Mzunguko wa 32 utamalizika Jumanne 25-04-17 Miembeni SC v/s Kilimani City FC Amani saa 8:00 mchana, na saa 10:00 za
jioni KVZ v/s Black Sailors na saa 1:00 Usiku Derby ya Jangombe kati ya Jang’ombe
Boys FC v/s Taifa ya Jang’ombe.
Comments
Post a Comment