Jina lake ni Khamis Mussa “Rais” ambae hadi leo bado rekodi yake haijavunjwa na mchezaji yoyote kwenye mechi ya Dabi ya Jang’ombe kati ya Jang’ombe Boys dhidi ya Taifa ya Jang’ombe. Ni Striker hatari wa Jang’ombe Boys, huyu jamaa ndiye mchezaji aliyefunga magoli mengi zilipokutana timu hizo. Ameshafunga mabao mawili mpaka sasa na hakuna mwengine yeyote alifika mabao hayo. Rais amefunga mabao hayo katika mchezo mmoja wa mzunguko wa kwanza wa ligi kuu soka ya Zanzibar kanda ya Unguja ambapo timu hizo zilitoka sare ya kufungana mabao 2-2 mchezo uliopigwa katika Uwanja wa Amaan siku ya Jumamosi ya Disemba 10, 2016. Mabao hayo alifunga katika dakika ya 45 na 53 huku akimuweka katika wakati mgumu mlinda mlango hatari wa Taifa ya Jang’ombe Ahmed Ali “Salula”. Wachezaji wengine ambao wanaweza kuivunja rikodi hiyo kwa upande wa timu ya Taifa ni Mkongo Baraka Ushindi, Mkenya Mohd Said “Mess”, Omar Yussuf Chande na Hassan Seif “Banda” ambao wote wamefunga bao moja tu. RIKODI USO...
K ocha mkuu wa timu ya taifa ‘Taifa Stars’ Salum Mayanga ametangaza kikosi cha wachezaji 23 ambao wataingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya michezo miwili ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya DR Congo na Algeria. Wachezaji wa tano wa Zanzibar ni mlinda mlango Abdulrahman Mohamed wa JKU, pamoja na viungo Mudathir Yahaya wa Singida United, Feisal Salum wa JKU, Abdulaziz Makame wa Taifa ya Jang’ombe na Mohamed Issa wa Mtibwa Sugar. Kikosi kamili kilichotangazwa na Mayanga kinajumuisha wachezaji wafuatao: Magolikipa ni Aishi Manula, Abdulrahman Mohamed na Ramadhani Kabwili. Walinzi: Shomari Kapombe, Hassan Kessy, Gadiel Michael, Kelvin Yondani, Erasto Nyoni na Abdi Banda. Viungo: Hamisi Abdallah, Mudathir Yahaya, Said Ndemla, Feisal Salum, Abdulaziz Makame, Mohamed Issa, Thomas Ulimwengu, Farid Mussa, Shiza Kichuya, Ibrahim Ajib. Washambuliaji: Mbwana Samatta, John Bocco, Simon Msuva na Yahaya Zayd. Mara ya mwisho Mayanga alitaja kikosi cha Stars Oktoba 24,...
Kikosi maalum cha kuzuia magendo Zanzibar (KMKM) kimeandaa mashindano ya mbio za kilomita 10 ambazo zinatarajiwa kufanyika Jumapili ya Oktoba 29 mwaka huu zitakazoanza Makao Makuu ya KMKM Kibweni na kumalizia katika Viwanja vya Maisara. Akizungumzia lengo la Mashindano hayo CDR Hussein Mohd Seif ambae ni mkuu wa Mafunzo na Michezo KMKM amesema kila mwaka wanaandaa mashindano hayo kwaajili ya kujenga mahusiano ya karibu kati ya KMKM na jamii. Nae Mwenyekiti wa Chama cha Riadha Zanzibar Abdulhakim Cosmas Chasama amewapongeza KMKM kwa kuendeleza Mashindano hayo kila mwaka kwani yanaibua vipaji vingi katika mchezo huo.
Comments
Post a Comment