MIEMBENI CITY YAITAKA LIGI KUU KWA HAMU KUBWA
Timu ya Miembeni city imefanikiwa kupata alama tatu muhimu
jioni ya leo baada ya kuifunga timu ya Sebleni United katika mchezo wa 4 bora
ligi daraja la kwanza Taifa uliopigwa katika Uwanja wa Amaan.
Katika mchezo huo ambao ulikuwa na upinzani mkubwa mabao ya
Miembeni City yamefungwa na Ahmed Keis dakika ya 79 na Issa Chitwanga dakika ya
84.
Mchezo mwengine umepigwa saa 1 za usiku katika uwanja huo wa
Amaan ambapo timu ya Charawe ikafanikiwa kupata ushindi wa mabao 4-2.
Kwa matokeo hayo Miembeni City imezidi kujipa matumaini ya
kupanda ligi kuu msimu ujao ambapo wakifanikiwa kupita hapo watakutana na timu
nyengine ambazo zitabakia kwenye ligi kuu msimu huu pamoja na wao wanne wawili
kutoka Pemba na wawili Unguja ili kupanga mfumo gani watumie kupatikana timu 12
za ligi kuu msimu ujao.
City mchezo wa awali waliichapa Charawe mabao 2-0 ambapo
mpaka sasa wanaongoza wakiwa na alama 6 kwa michezo miwili huku Charawe
ikishika nafasi ya pili kwa alama 3 na Ngome ikishika nafasi ya tatu pia ikiwa
na alama 3 huku Sebleni United ikifuta matumaini ya kucheza ligi kuu msimu ujao
kufuatia kufungwa michezo yote miwili ambapo wa awali ilichapwa 2-1 na Ngombe.
Michezo ya mwisho itapigwa Mei 9, 2017 ambapo saa 10:00 za
jioni kumi watasukumana Sebleni United dhidi ya Charawe na saa 1:00 za usiku
Miembeni City watamalizana na Ngome michezo yote itachezwa katika uwanja wa
Amani mjini Unguja.
Wachezaji wa Miembeni City |
Comments
Post a Comment