MIEMBENI WATIA AIBU LIGI KUU ZENJ, WAFIKA UWANJANI NA WACHEZAJI 9 TU

Timu ya Miembeni wazee wa kwala leo imeonesha kituko katika mchezo wa ligi kuu soka ya Zanzibar kanda ya Unguja baada ya kufika kiwanjani hapo wakiwa wachezaji 8 pekee.

Mchezo huo uliopigwa majira ya saa 8 za mchana katika uwanja wa Amaan ambapo Kwala walikuwa wanacheza na Mafunzo.

Mchezo umeanza huku Miembeni wakiwa pungufu (9) na baadae wakatimia 11, wakaenda mapumziko Mafunzo 3-0 Miembeni .

Waliporudi kipindi cha pili wakaingia 8 wakacheza mchezo huo mpaka dakika ya 54 Miembeni wakabakia wachezaji 6 uwanjani kufuatia wachezaji wake wengine wawili kushindwa kuendelea na mchezo, ndipo hapo Muamuzi Mfaume Ali Nassor kulazimika kuuvunja mchezo huo huku Mafunzo akiwa mbele kwa mabao 4-0.

Mchezo mwengine umepigwa saa 10 za jioni ambapo JKU akaifunga Mundu mabao 4-0.

Ligi hiyo itaendelea tena Jumanne.

J/nne 02/5 Chwaka vs Zimamoto saa 8:00 Amaan
J/nne 02/5 B/Sailors vs Kimbunga saa 10:00 Amaan
J/nne 02/5 Kilimani C vs J/Boys saa 1:00 usiku.

Jumatano 3/5 KMKM vs Malindi saa 8:00 Amaan.
Jumatano 3/5 Kipanga vs KVZ saa 10:00  Amaan.

Comments

Popular posts from this blog

HUYU NDIYE MCHEZAJI MWENYE REKODI YA KUFUNGA MAGOLI MENGI KWENYE MECHI YA TAIFA DHIDI YA BOYS

WACHEZAJI WA 5 WA ZANZIBAR HEROES WAMEITWA TIMU YA TAIFA YA TANZANIA TAIFA STARS KWAAJILI YA MICHEZO MIWILI YA KIMATAIFA YA KALENDA YA FIFA.

KMKM KUANDAA MASHINDANO YA RIADHA