MUNDU YAKUMBUKA SHUKA WAKATI TAYARI KUMEKUCHA, KESHO HOMA YA JIJI KATI YA TAIFA NA BOYS
Timu ya Mundu kutoka Nungwi Kaskazini ya Unguja leo imefanikiwa kupata ushindi wa mabao 4-2 walipoichapa Chwaka Stars kwenye mchezo wa ligi kuu soka ya kanda ya Unguja mchezo uliopigwa atika uwanja wa Amaan saa 10 za jioni.
Mabao ya Mundu yamefungwa na Abas Pele (Hat trik) dakika ya 55, 60,82 na Yahya Shaaban dakika ya 63.
Mabao ya Chwaka Stars yamefungwa na Hisan Abdallah dakika ya 11 na Ibrahim Sultan dakika ya 51.
Leo saa 1 za usiku Zimamoto dhidi ya Polisi katika Uwanja wa Amaan.
Ligi hiyo itaendelea tena kesho kwa kupigwa michezo mitatu katika uwanja wa Aman.
Saa 8 za mchana Miembeni dhidi ya Kilimani City, saa 10 KVZ dhidi ya Black Sailors, na usiku homa ya jiji kati ya Taifa ya Jang'ombe na ndugu zao Jang'ombe Boys.
Comments
Post a Comment