RAIS WA BOYS AVUNJA REKODI YAKE MWENYEWE, NA NDIE MCHEZAJI ALIYEMFUNGA MABAO MENGI KIPA SALULA WA TAIFA
Mshambuliaji hatari wa timu ya Soka ya Jang’ombe Boys Khamis
Mussa (Rais) amevunja rekodi nyingine akiwa Boys katika Dabi ya Jang’ombe kati
ya Jang’ombe Boys dhidi ya Taifa ya Jang’ombe.
Goli alilofunga jana katika dakika ya 86 dhidi ya Taifa ya
Jang’ombe limemfanya kufikisha mabao matatu katika mchezo wa Dabi ya Jang’ombe
kati ya Jang’ombe Boys dhidi ya Taifa ya Jang’ombe akicheza katika dimba Amaan,
ambapo Boys kwa mara ya kwanza msimu huu wakiifunga Taifa baada ya kushinda 1-0.
Rais ameanza safari yake ya kufunga katika Dabi hiyo alipofunga
mabao mawili kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza wa ligi kuu soka ya Zanzibar
kanda ya Unguja ambapo timu hizo zilitoka sare ya kufungana mabao 2-2 mchezo
uliopigwa katika Uwanja wa Amaan siku ya Jumamosi ya Disemba 10, 2016.
Rikodi nyengine aloiweka Rais jana amekuwa mchezaji wa kwanza
kumfunga mabao mengi zaidi mlinda mlango hatari wa Taifa ya Jang’ombe Ahmed Ali
“Salula” baada ya kumfunga mabao matatu kwenye msimu huu.
Baada ya kufunga bao hilo pekee jana Rais amefurahi sana huku
akisema hafurahi kushinda yeye bao bali furaha yake kubwa ni kuwafunga Taifa
ambao wamekuwa wanawapa tabu sana wakikutana nao.
“Leo (Jana) ni siku ya furaha sana kwangu, ninafuraha mpaka
basi tena, sifurahi kushinda mimi bao, bali nafurahi kuwafunga Taifa, mana hao
wanakuwa wanatupa tabu sana tukikutana nao, mechi hii inakuwa na upinzani
mkubwa sana na mashabiki wanatoleana maneno mengi, sasa tumewaziba midomo, sisi
ndio Boys, umoja wetu ndio siri ya mafanikio”. Alisema Rais.
Comments
Post a Comment