TAIFA V/S BOYS ZIJUWE RIKODI ZAO WALIVYOKUTANA
Mchezo wa Dabi ya Jang’ombe wa ligi kuu soka ya Zanzibar kati
ya Taifa ya Jang’ombe dhidi ya Jang’ombe Boys utasukumwa kesho Jumanne saa 2:00
za usiku katika Uwanja wa Amaan.
Kikosi cha Taifa ya Jang'ombe |
Lakini Taifa katika Msimu huu wa mwaka 2016-2017 ameweka rikodi nzuri kwani mpaka sasa kwenye msimu huu wamekutana mara tatu na mbili Taifa kushinda na moja sare.
Huu ni mchezo wa 6 kukutana katika historia za timu hizi
ambapo katika michezo mitano waliyokutana Taifa alishinda miwili, na Boys
kushinda miwili na mmoja kutoka sare, hivyo mpaka sasa hakuna mbabe wapo sawa
na mchezo wa kesho ndio utatoa mwanya mzuri kwa timu itakayoshinda itakuwa
imeweka rikodi nzuri zaidi ya mwenziwe.
Kwenye mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo timu hizo zilitoka
sare ya kufungana mabao 2-2 mchezo uliopigwa katika Uwanja wa Amaan siku ya
Jumamosi ya Disemba 10, 2016.
Mabao ya Taifa siku hiyo alifunga Omar Yussuf Chande dakika 9
na Abdallah Mudhihir (Mido) dakika 60 wakati mabao ya Boys yote alifunga Khamis
Mussa (Rais) dakika ya 45 na 53.
Tarehe 19/11/2016 timu hizo zilikutana katika Bonanza maalum
la Coconut FM ambapo Boys kafungwa 2-0 na Taifa, mabao ambayo yalifungwa na
Mkongo Baraka Ushindi na Mkenya Mohd Said “Mess”.
Disemba 30, 2016 kwenye Kombe la Mapinduzi mchezo wa ufunguzi
Taifa alishinda 1-0 dhidi ya Boys bao pekee lililofungwa na Hassan Seif “Banda”.
Msimu wa Mwaka 2012-2013 Boys aliwafunga Taifa mara mbili wakati
huo timu zote zipo ligi Daraja la Pili Wilaya ya Mjini baada ya Boys kushinda
2-1 kwenye ligi hiyo, na mchezo mwengine Kombe la Waamuzi Boys tena kupata
ushindi baada kushinda kwa penalti 5-4 kufuatia dakika 90 kumalizika kwa sare
ya 0-0 michezo yote hiyo ilisukumwa katika Uwanja wa Mao Tsi Tung.
Hivyo tangu timu hizo zilipokutana kwenye Uwanja wa Amaan
msimu huu Taifa anarikodi nzuri ya kuifunga Boys kwani michezo yote mitatu
waliyocheza hapo Amaan Boys hajawahi kushinda kufuatia kufungwa miwili na
kwenda sare mmoja.
Comments
Post a Comment