TAIFA YA JANGOMBE LEO YAJIFARIJI, BADRU ASHUSHA PRESHA ZA MASHABIKI
Mzunguko wa 33 wa ligi kuu soka ya Zanzibar kanda ya Unguja umeanza jioni ya leo katika uwanja wa Amaan kwa kupigwa mchezo mmoja kati ya Taifa ya Jang'ombe dhidi ya Chuoni.
Katika pambano hilo Taifa amepata ushindi wa mabao 2-1.
Chuoni ndio wa kwanza kupata bao katika dakika ya 11 kupitia Ali Rajab, na bao hilo likadumu hadi kipindi cha kwanza kimemalizika.
Kipindi cha pili kuanza tu sekunde 35 Adam Ibrahim akarejesha bao hilo na dakika 59 Ali Badru akafunga bao la pili.
Ligi hiyo itaendelea tena kesho kwa kupigwa mchezo mmoja majira ya saa1 usiku kati ya Polisi dhidi ya Kijichi.
Comments
Post a Comment