TAIFA YA JANG’OMBE YAPIGWA FAINI KWA FUJO LA MASHABIKI WAKE KWENYE MCHEZO WA JANA
Timu ya Taifa ya Jang’ombe (Wakombozi wa Ng’ambo) imepigwa
faini ya Shilingi laki mbili kwa utovu wa nidhamu ambao umefanywa na Mashabiki
wake ambao wamerusha chupa za maji na kusababisha mpira kusimama kwa dakika 10
kwenye mchezo wa jana wa ligi kuu soka ya Zanzibar Kanda ya Unguja uliopigwa katika
Uwanja wa Amaan ambapo Taifa alifungwa bao 1-0.
Faini hiyo inatakiwa kulipwa si zaidi ya tarehe 4/5/2017 ambapo Maamuzi hayo yameamuliwa na
kamati Tendaji ya ZFA Unguja iliyokutana asubuhi ya leo.
Akizungumza na Mtandao huu Afisa Habari wa ZFA Ali Bakar “Cheupe”
amesema kamati Tendaji imeipitia ripoti ya mchezo huo kati ya Boys na Taifa na
kugunduwa kuwa Mashabiki wa Taifa wamefanya Utovu wa nidhamu.
“Kamati Tendaji ya ZFA imepitia ripoti ya mchezo huo na
katika ripoti hiyo imeripotiwa baadhi ya Mashabiki na Wapenzi wa timu ya Taifa
bila ya uhalali wowote wamefanya utovu wa nidhamu kwa kurusha chupa za maji na
kusababisha mpira kusimama, hivyo wamepigwa faini ya Shilingi laki mbili na
fedha hizo zinatakiwa kulipwa si zaidi ya tarehe 4/5/2017”. Alisema Cheupe.
Jeshi la Polisi likilazimika kuwatuliza Mashabiki kutorusha chupa |
Chupa ya Konyagi na ya Maji zilizorusha na Mashabiki Uwanjani |
Chupa ya Maji ndani yake ikitiwa Mkojo ambayo imerushwa na Mashabiki Uwanjani |
Comments
Post a Comment