WAUZAJI KARAFUU ZSTC WAWATIA ADABU WAZIMA UMEME ZECO MASHINDANO YA MEI MOSI
TIMU YA SHIRIKA la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC)
imefanikiwa kutwaa ubingwa wa mwaka huu 2017 wa Mashindano ya Mei Mosi baada ya
kuwafunga mabingwa Watetezi timu ya Shirika la umeme Zanzibar (ZECO) mabao 2-0
fainali ambayo imepigwa jioni ya leo katika Uwanja wa Amaan.
Mabao yote ya ZSTC yamefungwa na Majid Omar Majid ambae
alionesha makali yake katika mchezo huo ambao ulitawaliwa na mvua kiwanjani
hapo.
Katika Mashindano ya mwaka huu 2017 Mfungaji bora Bora
amefanikiwa kuwa Habibu Juma Ali aliyefunga mabao 5 katika Mashindano hayo, huku kipa bora akiwa Mbarouk Juma Ali wa
Shirika la Bandari na Muamuzi bora ni Juma Makame.
Comments
Post a Comment