AMOUR JANJA ATOKEA BENCHI NA KUPELEKA MSIBA JANG’OMBE BOYS
Na: Mossi Abdallah, Zanzibar.
Ligi kuu ya Zanzibar hatua ya 8 bora jioni ya leo imemaliza
mzunguko wa 3 kwenye dimba la Amaan ambapo Timu ya JKU imefanikiwa kutoka na
ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Jang’ombe Boys.
Mchezo huo ambao ulikuwa mgumu kwa timu zote mbili na
kupelekea hadi mapumzika hakuna timu iliyoona lango la mwenziwe.
Kurudi kumaliza kipindi cha pili timu zote zilifanya
mabadiliko kwa kila upande kutaka kuondoka na alama tatu muhimu lakini mchezaji
aliyetokea benchi Amour Omar “Janja” akaipatia alama tatu JKU baada ya kufunga
bao katika dakika ya 89 ya mchezo.
Comments
Post a Comment