BAZA KUMEKUCHA WAJIPANGA KUFANYA UCHAGUZI JUNE, WATAKA KUTEKELEZA AGIZO LA BTMZ
Kikosi cha Mafunzo cha Basket ball |
Chama cha Mpira wa Kikapu Zanzibar “BAZA” kipo mbioni kufanya Uchaguzi wake
ambao unatarajiwa kufanyika Mwezi wa June, 2017 ambapo mpaka sasa haujajulikanwa
utafanyika tarehe gani.
Akizungumza na Mtandao huu wa kisanduzenj.blogspot.com makamo
mwenyekiti wa BAZA Rashid Hamza amesema kwasasa wapo katika harakati za kufanya
uchaguzi wao ambao utafanyika mwishoni mwa mwezi wa June mwaka huu.
“Sasa tupo mbioni kufanya uchaguzi, na uchaguzi wetu
tunatarajia kufanya ndani ya mwezi wa sita, kwasasa tunaendelea na mchakato huo
na mambo yanakwenda vizuri mpaka muda huu”. Alisema Hamza.
Hivi karibuni BARAZA la Taifa la Michezo Zanzibar (BTMZ),
limeviagiza vyama vya michezo ambavyo
havijafanya uchaguzi kufanya hivyo ili
kupata viongozi kulingana na katiba zao ili waongoze kwa demokrasia na kwa kufuata
katiba.
Vyama vitano (5) ambavyo vinaharakishwa kufanya uchaguzi
ndani ya mwezi June, 2017 ni Chama cha Basketball Zanzibar (BAZA), Chama cha
Baskeli Zanzibar (CHABAZA), Chama cha Mpira wa Netball Zanzibar (CHANEZA),
Chama cha Mpira wa Mikono Zanzibar yani Hand ball na Chama cha Mpira wa Meza
Zanzibar yani Table Tennis.
Comments
Post a Comment