COCA-COLA YAZIPIGA JEKI SHULE ZA SEKONDARI ZANZIBAR KWA KUWAPATIA JEZI NA MIPIRA
Kampuni ya vinyaji baridi ya Cocacola imetoa Vifaa vya
Michezo vikiwemo jezi na mipira kwa ajili ya Skuli za Sekondari 251 za Unguja
na Pemba kwa ajili ya michezo ya soka na mpira wa kikapu, pamoja na mashindano
ya UMISSETA ambayo yatakayofanyika kuanzia June 6, 2017 huko Butimba Mkoani Mwanza ambapo
Zanzibar mwaka huu zitatoa kanda mbili
tofauti, Kanda ya Unguja na Kanda ya Pemba.
Vifaa hivyo vimekabidhiwa na Waziri wa Habari, Utalii,
Utamduni na Michezo Rashid Ali Juma ambae ndie aliyekuwa mgeni rasmi na ameipongeza
kampuni hiyo kwa kuthamini Michezo huku akisisitiza kuvithamini na kuvitunza
vifaa hivyo.
Mbali ya Vifaa hivyo pia Kampuni hiyo imetoa Vinywaji vya Coca cola kwa Wanafunzi na Wananchi wote waliyofika Uwanjani hapo Amaan kwenye hafla hiyo.
Afisa masoko msaidizi wa kampuni ya Cocacola Pamela Lugenge
Comments
Post a Comment