HONGERA MZENJ KOCHA BUSHIR KUISAIDIA MWADUI KUSHINDA TUZO TIMU YENYE NIDHAMU
Timu yenye nidhamu kwenye ligi kuu msimu uliomalizika ni Mwadui FC ya Shinyanga ambayo imepata zawadi ya Sh. 17.5 milioni.
Timu hiyo inafundishwa na Mzanzibar Ali Bushir "Bush" ambae alitoka KMKM ya Zanzibar.
Bush kwenye ufundishaji wake huwa yupo makini na nidhamu tangu alipokuwa Mlinda Mlango wakati alipokuwa akicheza mpaka kuwa Mwalimu na leo timu yake imefanikiwa kuwa ndio timu pekee yenye nidhamu kwenye timu 16 zilizoshiriki ligi kuu soka Tanzania bara msimu wa mwaka 2016-2017.
Blog hii inampongeza kocha Bush.
Hongera Sana Coach Ali Bush na sisi Kilimani City pia tunakupongeza na kukutakia mafanikio zaidi na zaidi
ReplyDelete