ILE MECHI ILIYOSHINDWA KUMALIZWA JANA PENALTI BAADA YA KUINGIA GIZA, HATIMAE LEO IMEMALIZWA KWA KUPIGWA PENALTI MOJA TU NA IPA KUUNGANA NA ZU, AFYA NA ZIFA NUSU FAINALI ZAHILFE
Timu ya soka ya Chuo cha Utawala wa Umma Zanzibar (IPA) leo
imetinga hatua ya nusu fainali kwenye Mashindano ya Vyuo Vikuu na Taasisi za
Elimu ya Juu Zanzibar baada ya kushinda penalty 1-0 dhidi ya SUMAIT kufuatia
mchezo huo kuendelezwa mchana wa leo kwenye dimba la Amaan.
Mchezo huo ni muendelezo kufuatia jana kutoka sare ya 2-2
ndani ya dakika ya 90 katika uwanja wa Fuoni kisha kupigiana mikwaju ya penalti
6 na kutoka sare ya 5-5 kufuatia kila timu kukosa penalti1 na kupata 5.
Pambano likalazimika kulazwa jana na kuendelezwa leo kwa
mikwaju ya penalti na iliendelea penalti moja moja kwa kila timu ambapo SUMAIT
walikosa na IPA wakapata, hivyo IPA wametinga nusu fainali kwa ushindi wa jumla
ya penalti 6-5.
Nusu fainali ya Mashindano hayo zitapigwa kesho majira ya saa
10:00 za jioni katika Viwanja Viwili tofauti.
Comments
Post a Comment