JANG’OMBE BOYS YAPATA SHAVU KUCHEZA SPORTPESA SUPER CUP, WATASHINDANA NA KINA YANGA, SIMBA, SINGIDA UNITED, GOR MAHIA, NAKURU ALL STAR NA LEOPARD
Timu ya Soka ya Jang’ombe Boys inayoshiriki ligi kuu soka ya
Zanzibar imepata bahati ya kuwemo kwenye Mashindano ya Sport Pesa Cup yanayotarajiwa kuanza kutimu
vumbi June 5, 2017 jijini Dar es salam.
Ligi hiyo itashirikisha jumla ya timu 8 kutoka Tanzania na
Kenya ambayo itachezwa kutafuta bingwa na mshindi wa pili.
“Ni kweli kwa hapa Zanzibar Jang’ombe Boys pekee wamepata
mualiko kucheza Ligi hiyo ambayo itahusisha vilabu vikubwa vya Bara na Kenya”.
Kilieleza chanzo.
RATIBA KAMILI HIYO
5/6/2017
Singida united Vs FC leopard
Yanga Vs Tusker fc
6/6/2017
Simba Vs Nakuru All Star
Jang`ombe boys vs Gor mahia
Nusu fainali tarehe 8/6/2017
Bingwa wa mechi kati ya Singida united vs AFC leopard
atacheza na bingwa kati ya Yanga na Tusker.
Nusu fainali ya pili Bingwa wa mechi kati ya Simba na Nakuru all-star
atacheza na bingwa wa mechi kati ya Jangombe boyz na Gor mahia
Fainali ni tarehe 11/6/2017 ambapo Bingwa wa SportPesa Super
Cup ataondoka na kitita cha dola 30,000 huku mshindi wa pili akipata dola
10,000.
Kila la kheri Boys tunawaombea ushindi na ni icon kwa Zanzibar hivi sassa
ReplyDelete