KIKOSI CHA UMISSETA KANDA YA UNGUJA KITAKACHOKWENDA MWANZA KIMEPATIKANA
Kocha msaidizi wa timu ya soka Kanda ya Unguja Abdul wahab
Dau “Mwalimu Dau” ametangaza kikosi kipya wachezaji 21 cha timu hiyo ambacho
kinatarajiwa kwenda Butimba Jijini Mwanza
katika Mashindano ya Umoja wa Michezo na Sanaa Shule za Sekondari
Tanzania (UMISSETA)yanayotarajiwa kuanza
June 6, 2017.
Kikosi hicho kinatarajia kuondoka Visiwani Zanzibar siku ya
Jumamosi ya June 3, 2017.
WALINDA MLANGO
Aley Ali Suleiman (Ubago) na Ali Makame (Muembe ladu)
WALINZI
Ibrahim Abdallah Hamad (Arahman), Abdurahman Seif Bausi (Glorious),
Abubakar Khamis (Bububu), Abdul aziz Ameir Khatib (Arahman), Ali Issa Omar (Lumumba), Ahmed Mohd Shaaban (Nyuki) na Abbas Yahya.
VIUNGO
Amani Ali Suleiman (Kiembe Samaki), Ibrahim Faraj “Mess” (Lumumba), Haji
Suleiman (JKU Mtoni), Yakoub Kiparo (Langoni), Jamali Ali Jaku “Ozil” (Kinuni)
na Eliyasa Suleiman (K-pura).
WASHAMBULIAJI
Faki Kombo (JKU Mtoni), Mundhir Abdallah (JKU Mtoni), Ali
Hassan (Bububu), Walid Abdi “Pato” (Mwera), Ali Mohd Seif (Tumekuja) na Ali
Omar (Mwera).
Mashindano ya UMISSETA yanayotarajiwa kuanza June 6, 2017
huko Chuo cha Ualimu Butimba Mkoani Mwanza ambapo kwa mwaka huu Zanzibar
itashiriki kanda mbili tofauti, yani Kanda ya Unguja na Kanda ya Pemba.
Comments
Post a Comment