KOMBAIN YA MJINI YA ROLLING STONE YAZIDI KUSUKWA UPYA, SASA WAPO 30 WA UHAKIKA AKIWEMO ABUU LUIZ WA CITY
Mabingwa watetezi wa
Mashindano ya Vijana ya Rolling Stone kombain ya Mjini Unguja ambayo inaandaliwa na Kocha Mohammed Seif “King”
kwenda jijini Arusha kwenye Mashindano ya Vijana ya Rolling Stone ambayo
yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi lake kuanzia June 29, 2017 na kumalizika July
9, 2017.
Kwa mujibu wa kocha King uteuzi wa kuchagua wachezaji
umefikia tamati na hakuna atakaengezwa tena baada ya kufika jumla ya Wachezaji
30 ambapo watachujwa 6 na kubakia 24 ambao ndio watakaokwenda katika Mashindano
hayo.
Wachezaji 30 ni :-
WALINDA MLANGO
Aley Ali Suleiman
“Manula” (Miembeni city), Peter Dotto Mashauri (Schalke 04), Makame Mkadar Koyo
(Huru) na Ibrahim Abdallah Ali “Parapanda” (Amani Fresh).
WALINZI WA PEMBENI
Muharami Khamis “Terra” (Black Sailors), Abdul hamid Salum
“Ramos” (KVZ), Hassan Chalii (Kipanga), Abdul-halim Ameir (King Boys), Ali
Hassan (Uhamiaji),
WALINZI WA KATI
Ali Juma Maarifa “Mabata” (Taifa ya Jang’ombe), Shaaban Pandu
“Brown” (Villa United), Ismail Mcha (Muembe Beni), na Abubakar Ame “Luiz” (Membeni
City).
VIUNGO WA KATI
Assad Juma “Hussein Deco” (Kilimani City), Mussa Shaabani
(Zimamoto), Fahmi Salum (Mlandege), Salum Omar “Carrick” (Villa United), Ibrahim
Chafu (Villa FC) Yakoub Omar (Jang’ombe Boys), Mohd Ridhaa (Villa United),
Yussuf Mohd (Muembe Beni), Talib Khamis (Kipanga) na Suleiman De Jong.
VIUNGO WA PEMBENI
Abrahman Juma “Baby” (KMKM), Mohd Jailan (Chrisc), Mohd Haji
(Jang’ombe Boys) na Suleiman Doredo.
WASHAMBULIAJI
Ibrahim Abdallah “Imu Mkoko” (Miembeni City), Mohd Mussa
(Mapembeani) na Juma Ali Yussuf “James” (Villa United).
Comments
Post a Comment